Friday, July 6, 2012

BAADA YA MSECHU KULALAMIKA, DAMIAN AZUNGUMZA UKWELI.

Wa kwanza kulia ni Mtanzania Damian staa wa single ya hakuna matata ambae jumatano July 4 2012 ametoa single mpya inaitwa Taratibu.
                                                          Peter Msechu wa tatu kutoka kushoto.
Kama ulifatilia, stori ya aliyekua mshiriki wa Tusker Project Fame Peter Msechu wiki iliyopita kuhusu kulalamikia washiriki wa Tanzania kutolewa kwenye Tusker Project mwaka huu, hatimae mmoja kati ya walengwa hao amekubali kuzungumza kilichotokea.

Msechu alilalamikia wawakilishi wote wawili wa Tanzania Project fame kutolewa na kuifanya Tanzania kuwa nchi ya kwanza washiriki wake wote kutolewa mwaka huu.

Alisema “walijiamini kupitiliza, siku  Imani Lissu ameingia kwenye kipindi cha hatari cha kutolewa kulikua na time kwa washiriki waliobaki kumchagua mshiriki gani abaki kwa kupiga kura lakini ukiangalia Damian kama Mtanzania hakumpigia kura mtanzania mwenzake kubaki angalau hata kuonyesha ule uzalendo, sasa hiyo kwa mimi ambae nimeshiriki tulikua tukionywa sasa sijui mwaka huu kama hawakuonywa?

Kwenye sentensi ya pili Msechu alisema “Kwa Damian ambae ndio alibaki kuiwakilisha Tanzania Tusker Project mahojiano ambayo aliyafanya baada ya kuingia kwenye kipindi cha hatari cha kuomba kura mwisho wa siku alisema hawa majaji walionifanya niingie kwenye kipindi cha hatari walifanya maamuzi mabovu”

Damian alisema maneno yafuatayo “by the way ule ni mchezo tu kwa sababu vitu vingine tunapangwa, kunakua na muongozaji ambae anasimamia hizo ishu, unapewa Idea za nini cha kufanya ili kuchochea kitu fulani, hausemi vile kwa mtazamo wako kwamba Majaji wamekosea, unaambiwa cha kufanya ili kuifanya Tusker Project iwe stori zaidi…. mimi niliikubali hiyo idea kwa sababu walinipa sababu kwamba unajiweka sokoni wewe mwenyewe kwa hiyo lazima uonyeshe kwamba wewe sio dhaifu, ambapo mwongozaji alisema pia kwamba tunatakiwa tuwape majaji upinzani, sio kufika mbele yao tu na kila kitu unasema asante… lakini unaweza kuwauliza maswali unaweza kuwaambia chochote majaji kwa hiyo ile kuongea vile ilikua sehemu ya mchezo” Chanzo: millardayo.com

No comments: