Friday, July 6, 2012

THEA AJIFUNGUA MTOTO SIYO RIZIKI

MSANII mwenye heshima kunako tasnia ya filamu za Bongo, Ndumbangwe Misayo ‘Thea’ (pichani) amejifungua lakini mtoto wake akiwa amefariki dunia.

Chanzo chetu makini kilichoomba hifadhi ya jina lake kilieleza kuwa, Thea alijifungua mtoto wa kike kwa njia ya kawaida usiku wa kuamkia Jumanne iliyopita katika Hospitali ya Marie Stopes lakini akawa siyo riziki.

“Unajua familia yao haikutaka mapaparazi wajue kuwa Thea yupo hospitali kwa ajili ya kujifungua kwa sababu hawapendi magazeti hivyo hapa nimefanya kuwaambia tu msinitaje jamani,” kilisema chanzo hicho.

Aidha, chanzo hicho kiliongeza kuwa mwili wa kichanga hicho ulizikwa katika Makaburi ya Mwananyamala jijini Dar juzi Jumanne asubuhi.

Jitihada za kuwapata Thea au mumewe Mike Sangu ili kuzungumzia ishu hiyo hazikuzaa matunda.
Tanzania Asilialive.blogspot.com  inawapa pole sana Mr na Mrs Sangu Tunaamini yote ni mipango ya mungu poleni sana.

Chazo: Globalpublishers

No comments: