Monday, July 9, 2012

Timu Ya Taifa Ya Olimpiki Inaondoka Leo Kwenda Nchini Uingereza

Timu ya Taifa ya Olimpiki inaondoka leo kwenda nchini Uingereza kushiriki michezo ya 30 ya Olimpiki itakayofanyika jijini London. Wachezaji watakaoondoka ni pamoja na wanariadha Samson Ramadhan, Mohamed Msindoki, Faustine Mussa (marathon) na Zakhia Mrisho anayekimbia mita 5,000. Pia Bondia pekee katika safari hiyo ni Seleman Kidunda, kwa upande wa kuogelea utawakilishwa na Magdalena Moshi.

No comments: