Friday, September 28, 2012

CUF YASHUTUMU WAFUASI WA CHADEMA KWA KUSHAMBULIA WAFUASI WAKE KATIKA VURUGU ZA ARUSHA






Angalia picha jinsi ya mambo yalivyokuwa wakati wamachinga wa jijini Arusha walivyopora kiwanja na kuanza kujipimia ili kufanyia biashara kabla ya polisi kuinguilia kati


CHAMA Cha Watu wananchi CUF kimetoa tamko kali kwa kuwatuhumu wafuasi sita wa Chadema jijini Arusha kwamba walihusika na vurugu za kulishambulia gari la matangazo na kisha kumpiga mawe mfuasi wao huku wakilitaka jeshi la polisi kuchukua hatua kali za kisheria.

 Akitoa tamko hilo leo  katika ofisi za chama hicho zilizopo kata ya Kaloleni jijini Arusha,mjumbe wa baraza kuu la uongozi taifa wa CUF, Mbarala Maharagande, alisema kwamba chama chao kina ushahidi  wa kutosha kwamba mfuasi wao, Athuman Abdulraham, alipigwa mawe na wafuasi wa Chadema wakati akiwa katika gari la matangazo.

Maharagande,alisema kwamba mfuasi wao alikuwa katika eneo la Levolosi karibu na eneo lililovamiwa na wamachinga na wakati akiwa ndani ya gari hilo wafuasi wa Chadema walianza kumyooshea alama ya vidole viwili kabla ya kuanza kumpopoa kwa mawe.

Hatahivyo,alisisitiza kwamba tayari mfuasi huyo ameshatoa tarifa kwa jeshi la spolisi mkoani hapa na kufungua faili nambari AR/RB/12419/012 na kulitaka jeshi hilo kuwakamata wafuasi hao wa Chadema  hadi kufikia septamba 30 mwaka huu na wakishindwa wao watachukua  hatua za kisheria wanazozijua.

 “Kijana amepigwa na wafuasi wa Chadema na tayari tunawajua wako sita tumeshatoa tarifa polisi wawachukulie hatua na kama wakishindwa basi sisi tutachukua hatua za kisheria tunazozijua”alisema Maharagande

 Alisema kwamba wana tarifa za kutosha kwamba Chadema wamefanya vurugu za kutaka kuharibu mkutano wa hadhara wa chama chao unaotaraji kuhudhuriwa na mwenyekiti wake,Prof Ibrahim Lipumba sanjari na makamu mwa kwanza wa Rais Zanzibar,Maalim Seif Sharif Hamad .

 Alisema kwamba wao wamekuja Arusha kufanya kazi za siasa zikiwa ni pamoja na kujiandaa na uchaguzi wa madiwani,ubunge pamoja na kueneza serĂ¡ ya V4C iliyoasisiwa hivi karibuni.

 Hatahivyo,alisisitiza kwamba wao hawapendi kupambana na Chadema kwa kuwa hawana serikali huku akisisitiza kuwa kama ni fujo wanazijua lakini kwa sasa wanaeneza serĂ¡ na kama Chadema wakitaka kupambana nao wakashindane kwa hoja majukwaani.

No comments: