Friday, September 28, 2012

Ufafanuzi wa kilichotokea Uchaguzi Meya Mwanza..CCM Yafanya "UMAFIA"

CCM wameshindishwa na mbinu za kisiasa amabzo uhalali wake kisheria linabaki kuwa suala la wanasheria wanaojua taratiu zikoje.

Baada ya mgawanyo wa h/shauri ya jiji na kuwa na h/shauri ya jiji inayoundwa na jimbo la Nyamagana na halmashauri ya ilemela inayondwa na jimbo la ilemela mwezi Julai mwaka huu mgawanyo wa madiwai ulikuwa hivi kwa nyamagana

Chadema -wa kata 5, viti ,maalum 2. mbunge mmoja, jumla wanakuwa 8
CCM - wa kata 6, viti maalum 1 jumla wanakuwa 7
Cuf - wa kata 1, viti maalum 1

Ilemela

Chadema -- wak kata 6, viti maalum 2 mbunge 1 jumla wanakuwa 9
CCM - wa kata 3, viti maalum 2 na mbunge 1 (wa viti maalum) jumla wanakuwa 6
CUF - MBUNGE WA viti maalum 1

Kilchotokea kwenye uchaguzi ni CCM kuhamisha diwani mmoja wa viti maalum (kwa barua ya CCM kwenda kwa mkurugenzi wa jiji ya tarehe 14, Septemba, 2012) na mbunge wa viti maalum toka Ilemela kuja nyamagana na hivyo kuongeza idadi ya kura zao kuwa 9, wakati huo huo Chadema walishakuwa hawaihehabu kura ya Diwani wa Igoma Chagulani ambaye wamemfukuza uanachama akalejeshewa na mahakama wao wanapugukiwa na kura 1 zao zinabaki 7 , aliyepungua Chadema akiwapigia CCM wanakuwa na kura 10 dhid ya 7 za Chadema.

Lakini pia CUF walishakubaliana na chadema kuungana mkono, kwa hiyo kwa kura 2 za CUF Chadema wangekuwa na kura 9, lakini inaonekana ama mwana Chadema mmoja kapigia CCM au CUF mmoja kapigia CCM na kufanya matokeo ya kuwa kuwa 11 kwa CCM dhidi ya nane za Chadema.

Hiyo ndiyo hali halisi ya jinsi mahesau ya kura yalivyochezwa, kama kuna uhalali katika mchakato huo au la ni suala la wataalamu wa masuala haya kutujuza.

Hayo yakiendelea uchaguzi wa Meya wa Ilemela meahirshwa katika mazingira tata, baada ya Mkurugeni kusoma Amri ya Mahakama iliyopewa tafsiri na mwanasheria wa jiji kuwa inakifanya kikao hicho kuahirishwa kwa kuwa Diwani wa Chadema Matata (pia alifukuzwa uanachama pamoja na wa igoma na anaendelea na udiwani kwa amri ya makahama) kuleta pia barua ya kutaka atambuliwe kaa mgombea.

Ukazuka ubishi kidogo juu ya hoja ya mgombea kuteuliwa na chama, mkurugenzi wa jiji akasema hiyo siyo sheria ni mwogozo, na kwa kuwa sheria na mwongozo zikigongana sheria ndiyo inatamalaki hatakia aingie katka mgogoro wa tafsiri ya sheria, akaahirisha kikao bila hata madiwani kujadili hoja hiyo.

Kwa mujibu wa mwanasheria wa wa Chadema, pingamizi hilo lilikuwa linawarejeshea haki yao ya uanachama na hivyo kuendelea na udiwani wao, na kutaka matata asizuiliwe kuendelea na mchakato wa kuomba umeya, Kwa hiyo matata ameomba lakini hakuteuliwa na chama na mahakama haiwezi kuwalazmisha chama wateue mgombea kwa amri ya mahakama, anadhani ni uhuni tu na njama za kisiasa zimefanyika kuahirisha uchaguzi huo.
Nadhani kidogo piacha itaeleweka kwa wanjamvi juu ya nini hasa kimetokea.

SOURCE: Kamnada Deus Bugaywa-Mchambuzi Raia Mwema

No comments: