Monday, November 12, 2012

Hotuba Ya JK Kwenye Mkutano Mkuu Wa CCM Dodoma

HOTUBA YA MHE. JAKAYA MRISHO KIKWETE, RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA NA MWENYEKITI WA CCM KWENYE UFUNGUZI WA MKUTANO MKUU WA NANE WA CHAMA CHA MAPINDUZI, UKUMBI WA KIZOTA – DODOMA, TAREHE 11 NOVEMBA, 2012

Utangulizi Mheshimiwa Dkt. Amani Abeid Karume, Makamu Mwenyekiti wa CCM na Rais Mstaafu wa Zanzibar; Ndugu Pius Msekwa, Makamu Mwenykiti wa CCM wa Bara; Mwenyekiti Mstaafu wa CCM,

Ndugu Benjamin William Mkapa; Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi; Waziri Mkuu; Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ;

 Viongozi Wakuu Wastaafu; Katibu Mkuu wa CCM, Ndugu Wilson Mukama; Ndugu Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Taifa wa CCM; Wageni wetu waalikwa kutoka vyama rafiki, Ndugu zetu wa Vyama vya Siasa Nchini; Waheshimiwa Mabalozi, Viongozi wa Dini, Wageni Waalikwa, Mabibi na Mabwana; Kama ilivyo ada, naomba tuanze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu, mwingi wa rehema kwa kutujaalia uzima na kutuwezesha kukutana hapa Dodoma, siku ya leo, kwenye Mkutano Mkuu wa Nane wa Chama cha Mapinduzi.

 Ndugu Wajumbe;

 Karibuni Dodoma. Karibuni Mkutanoni. Nawapeni pole kwa safari. Tunamshukuru Mungu kwa kutuwezesha kufika salama na tuombe turejee makwetu salama. Kwa niaba yenu, niruhusuni niwashukuru wenyeji wetu, yaani wana-CCM na wananchi wote wa Dodoma, wakiongozwa na Alhaji Adam Kimbisa, Mwenyekiti wa CCM, Mkoa wa Dodoma na Mkuu wa Mkoa Dkt. Rehema Nchimbi, Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa. Tunawashukuru kwa kutupokea vizuri na kwa ukarimu wao unaotufanya tujisikie tuko nyumbani katika huu mji ambao ndiyo Makao Makuu ya nchi yetu na Chama chetu.

Ndugu Wajumbe;

Napenda kuchukua nafasi hii kutoa pongezi nyingi kwa Halmashauri Kuu ya Taifa kwa matayarisho mazuri ya Mkutano huu wa Nane wa Taifa wa CCM. Natoa pongezi maalum kwa Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya Taifa chini ya uongozi mahiri wa Katibu Mkuu Ndugu Wilson Mukama na Kamati zote za Maandalizi ya Mkutano kwa kazi kubwa na nzuri waliyofanya ya kuwezesha Mkutano huu kufanyika. Kwenu nyote nasema hongereni na asanteni sana.

 Ndugu Wajumbe; Karibuni tena Kizota. Nasikitika kwamba .... Soma zaidi: http://www.kwanzajamii.com

No comments: