Friday, August 10, 2012

Mkazi wa Silent Inn afariki baada ya kugongwa na gari.

MKAZI mmoja wa eneo la Silent Inn aliyefahamika kwa jina la Bakari Sefu (35) amekufa baada ya kugongwa na gari .

Kamanda wa polisi mkoani hapa, Liberatus Sabas alisema kuwa tukio hilo limetokea wiki iliyopita  katika eneo la stand ndogo karibu na cafe la Aziz .

Alisema kuwa, chanzo cha ajali hiyo ni gari aina ya Nissan Caravan lenye namba za usajili T 278 BXD lililokuwa linaendeshwa na dereva ambaye bado hajafahamika jina lake baada ya dereva huyo kuondoa gari hilo kwa kasi.

Alisema kuwa, dereva huyo aliondoa gari hilo lililokuwa limeegeshwa likisubiri abiria ndipo lilipomgonga kondakta huyo ambaye alikuwa amesimama mbele ya gari hilo akiita abiria.

Sabas aliongeza kuwa, baada ya kusababisha ajali hiyo dereva huyo alikimbia na jeshi la polisi linaendelea kumsaka dereva huyo , huku mwili wa marehemu ukiwa umehifadhiwa katika hospitali ya mkoa ya Mount Meru.

No comments: