Monday, February 4, 2013

JK aongoza matembezi ya mshikamano

 Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Dk. Rais Jakaya Kikwete akiongoza  viongozi wengine wa chama katika  matembezi ya mshikamano yaliyofanyika leo mjini Kigoma  asubuhi.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye kulia akiwa na Edward katika matembezi hayo.

 Chama cha Mapinduzi CCM kinahitimisha sherehe hizo baada ya Sekretarieti yake ikiongozwa na Katibu Mkuu wa chama hicho Ndugu Abdurahman Kinana kufanya shughuli mbalimbali za kukagua miradi inayotekelezwa na Serikali mkoani Humo.
 Matembezi ya Mshikamano yakielekea ofisi ya CCM mkoani Kigoma


 Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Dk. Jakaya Kikwete akizungumza na wana CCM katika makao makuu ya CCM Mkoani Kigoma mara baada ya kumaliza Matembezi ya mshikamano ya kuadhimisha miaka 36 ya chama hicho yanayofikia kilele leo kwa  sherehe kubwa kwenye uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Dk. Rais Jakaya Kikwete akijiandaa pamoja na viongozi wengine wa chama wakijiandaa tayari kwa kuanza matembezi ya mshikamano mjini Kigoma leo asubuhi.

No comments: