Mh James Mbatia.

Waziri mkuu Mizengo Pinda amelazimika kuingilia kati mjadala wa wabunge kuhusiana na hoja iliyotolewa wakati wa mjadala wa mabadiliko ya sheria mbalimbali kuhusu kutoingiliwa kwa maamuzi yanayotolewa na wazee wa Mahakama kwenye baadhi ya mashauri yanayohusiana na masuala ya dini ya kiislam ikiwemo ndoa na mirathi.
Wakati hoja ikiendelea kabla ya kupitishwa kwake Waziri mkuu amesema ipo haja ya serikali kuliangalia upya hilo jambo na kutahadharisha kwamba huo mjadala ungeendelea ungeweza kuligawa taifa kwa misingi ya udini ishu ambayo ilisababisha mwanasheria mkuu wa serikali Jaji Frederick Werema kukifuta hicho kifungu.
Kwenye sentensi nyingine ni kwamba ishu ya mitaala ya elimu Tanzania iliendelea kumuandama mbunge wa kuteuliwa na rais Kikwete, James Mbatia baada ya mbunge wa Nzega Dk Khamis Kingwangalla kuomba muongozo wa spika kutoa hoja ya bunge kumwajibisha James Mbatia kwa kuongea uongo bungeni.
Namkariri Kigwangalla akisema “utaratibu uliovunjwa kwa mujibu wa kanuni ya 63 ni kusema uongo bungeni, imethibitika bila shaka yoyote kwamba Mh James Mbatia alilidanganya bunge, kwa kuwa alilidanganya bunge na kusema kwamba atakua tayari kujiuzulu mitaala hiyo ikiletwa”
No comments:
Post a Comment