Friday, February 8, 2013

MSIKUBALI KUDANGANYWA ANGALIENI MAFANIKIO YENU- PALANGYO

WANACHAMA wa Chama cha Mapinduzi wilaya ya Meru,mkoani Arusha,wameshauriwa kutokukubali kudanganywa na Vyama vya kisiasa ambavyo vinaeneza Propaganda chafu  kuwa hakuna kilichofanyika tangia Uhuru,badala yake wachukie siasa zinazosababisha uvunjifu wa amani


  Hayo yameelezwa na mjumbe wa kamati ya Siasa ya mkoa ya Chama cha Mapinduzi, John Palanjo, Februari 5 katika kilele cha maadhimisho ya miaka 36 ya CCM,yaliyofanyika katika eneo  Uwiro kata ya Ngarenanyuki Wilayani Meru Mkoani Arusha

Palanjo, aliwaambia wananchi kuwa umefika wakati kupuuza propaganda zinazoenezwa na Vyama vya kisiasa na badala yake waimarishe mshikamano miongoni mwao  kwa kuwa Chama cha Mapinduzi kina Ilani na ndoto ya kuboresha maisha ya watanzania.

Amewataka viongozi wa ngazi mbalimbali za Chama kuhakikisha wanatembelea wananchi na wanachama ili kusikiliza kero na kuzipatia ufumbuzi  sanjari na kufanya mikutano kila baada ya miezi mitatu kwa
mjibu wa katiba ya Chama ili kuhamasisha na kuimarisha uhai wa Chama.

Awali alisema kuwa viongozi nao wanatakiwa kujua na kutambua kuwa wao mtaji wa Chama cha Siasa ni watu, hivyo wafanye vikao na kuhamasisha watu wengi zaidi kujiunga na Chama cha Mapinduzi, na kuongeza idadi ya wanachama ambao watakiwezesha Chama kushinda katika chaguzi mbalimbali
zikiwemo za serikali za mitaa zitakazofanyika mwakani na uchaguzi mkuu mwaka 2015

Akitoa ufafanuzi wa kero ziliziopo kwenye Kata hiyo, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Meru, diwani Godson Majola, aliwahakikishia wananchi kuwa halmashauri ya wilaya ya Meru itaanza kuzitatua kero hizo ndani
ya muda mfupi

Amewataka  wananchi kuwa na subira pale ambapo baadhi ya kero hazitatatuliwa kwa muda mfupi kwa sababu kila jambo lina utaratibu wake na kuwataka wananchi wasipotoshwe wala wasiyumbe kwa propaganda za Vyama vya kisiasa hivyo wanainchi waimanini halmashauri yao kero zitapatiwa ufumbuzi

No comments: