Friday, February 8, 2013

KAMPUNI YA NDEGE YA fastjet YAKANUSHA UVUMI KUWA IMEFUTIWA LESENI YA BIASHARA

Jean Uku Meneja Masoko na Mauzo wa Kampuni ya ndege ya Fastjet akizungumza na waandishi wa habari kwenye hoteli ya Hyyat Regency Dar es salaam kukanusha uvumi wa habari zinazosema kampuni hiyo imenyang’anywa leseni ya kufanya biashari nchini Tanzania, Kushoto ni Givaldine Dawe Meneja Utawala.

Pamoja na habari zilizoandikwa na kusemwa kwenye vyombo vya habari leo, biashara ndani ya kampuni ya fastjet inaendelea kama kawaida. Madai yanayotukabili ya kunyang’anywa leseni hayana ukweli wowote. Tunaendelea kufanya kazi na ndege zetu nchini Tanzania kama kawaida na bado tunazidi kuzindua vituo vipya kama ilivyopangwa. Huu ni uzushi wa baadhi ya watu au kampuni zenye chuki dhidi ya kampuni ya fastjet, kusudi lao ni kudhoofisha uaminifu na kuharibu sifa ya jina la biashara na bidhaa zetu za fastjet.

Ofisi zetu na vituo vyetu vya kuuzia tiketi bado viko wazi kwa ajili ya bookings na Kwa tiketi zilizolipiwa pesa haitarudishwa.

TAMKO RASMI BAADA YA MASAA MACHACHE

Kwa mujibu wa taarifa zilizo potofu kutoka kwenye vyombo vya habari, David Lenigas, Mwenyekiti wa fastjet plc na Mwenyekiti wa Five Forty Aviation Limited (Kenya) (“FLY540 Kenya), anathibitisha kwamba hakuna Mikataba halali yoyote kati ya fastjet na fly540 juu ya jina la biashara au uongozi.
Kauli yaliyotolewa na Don Smith kutoka Kenya, mkurugenzi wa Fly540 Kenya, kupendekeza kuwa ana haki ya kuondoa jina la biashara sio jambo la kweli na halina msingi wowote.  Bodi ya Wakurugenzi wa Fly540 Kenya hawajawahi  kulifikiria suala hili.

fastjet ingependa kuvishauri vyombo vya habari na abiria wetu ambao wanaendelea kusafiri na ndege za fastjet na Fly540 barani Afrika, kwamba tunatarajia kupanua huduma zetu za gharama nafuu katika Bara la Afrika.

No comments: