Friday, March 22, 2013

"NAWASHANGAA WANAOPOTEZA MUDA KUYAFUATILIA MAISHA YANGU"....WEMA SEPETU

Msanii anayetafuta mafanikio kwa kasi, Wema  Sepetu amesema kuwa haoni sababu ya watu kutishiana maisha hasa kwa kipindi hiki ambacho maisha yapo juu.

Wema alisema hayo kufuatia hivi karibuni  kutishiwa maisha na watu asiowafahamu na  kulazimika kuongeza ulinzi nyumbani kwake na  kila anapokuwa anatoka.

Alisema maisha ni magumu na kila mmoja  anatakiwa afanye kazi kwa bidii ili kufikia  malengo, badala yake watu wanaanza kutishiana  maisha.

"Nawashangaa watu wanaoendelea kuwafuatafuata  wengine wanapata wapi ujasiri huo na hali ya  maisha ilivyo ngumu na kuhitaji muda mwingi wa  kufanya kazi ili kujikwamua,"alishangaa Wema.

Aidha, aliongeza kuwa hana adui wala mtu ambaye  anamdai au kitu kama hicho hivyo watu  wanaomtumia mesaji za vitisho anahisi wana chuki  binafsi na si kingine.

No comments: