Saturday, March 16, 2013

RAFIKI WA RAILA ODINGA AMPA TALAKA MKEWE KWA KUMSIFIA UHURU KENYATTA KUWA NI HANDSOME

 Rafiki wa karibu wa waziri mkuu wa Kenya Raila Odinga Jumatatu hii anadaiwa kumpa talaka mke wake baada ya kumsifia Rais mteule wa Kenya Uhuru Kenyatta ni ‘handsome’ mbele yake.

Kwa mujibu wa mtandao mmoja wa Kenya, mwanasiasa huyo wa chama cha CORD anayetokea magharibi mwa Kenya, alikuwa akitazama taarifa ya habari akiwa na mke wake na ndipo alipoonekena Uhuru Kenyatta kwenye TV akizungumza na wawakilishi wa nchi mbalimbali nyumbani wake.

Baada ya kumuona mke huyo ambaye ana miaka 30 na kitu alisikika akisema kwa sauti ya chini kuwa anapenda muonekano wa Uhuru Kenyatta.

Hata kabla hajamaliza neno Kenyatta, inadaiwa kuwa mwanaume huyo aliye na ukaribu na Raila Odinga, alimpa kichapo cha haja na kumfukuza nyumbani usiku huo.

Mke huyo ambaye anafanya kazi kama meneja wa benki alionekana kesho yake akihamisha vitu vyake huku mlinzi akimsaidia. Baadaye alionekana akiwa amebeba vitu alivyochukua kwenye lori akihama.

No comments: