Wednesday, March 6, 2013

Umoja wa Mataifa walaani vitendo vya kushambuliwa albino nchini Tanzania

 Umoja wa mataifa umelaani vikali vitendo vya kushambuliwa kikatili walemavu wa ngozi, albino nchini Tanzania kutokana na imani za kishirikina.

“Ninalaani vikali mauaji na mashambulio haya ambayo yamefanyika katika mazingira ya kutisha na ambayo yamehusishwa kukata viungo vya watu wakiwemi watoto wakati wakiwa hai,” alisema jana kamishna mkuu wa haki za binadamu wa umoja wa Navi Pillay.

“The killing and mutilation of people with albinism – a congenital disorder caused by the absence of pigment in the skin, hair and eyes – is often linked to witchcraft, yalisema maelezo yake.

Maelezo hayo yaliongeza: Baadhi ya watu wanaamini kuwa uchawi huwa na nguvu zaidi kama mhanga akipiga mayowe wakati akikatwa viungo, na ndio maana viungo vya mwili hunyofolewa kwa wahanga walio hai.
“Uhalifu huu unakera,” alisema Pillay.

January 31 mwaka huu mtoto wa miaka 7 Lugolola Bunzari aliuawa vikali katika kijiji cha Kanunge mkoani Tabora, alisema Pillay, mwanasheria wa Afrika Kusini ambaye aliwahi kuwa jaji wa mahakama ya kimataifa ya makosa ya jinai, ITC.

Aliongeza kuwa Maria Chambanenge, albino mwanamke mwenye miaka 39 alivamiwa February 11 na wanaume watano katika kijiji cha Mkowe mkoani Rukwa ambao walikamatwa baadaye.

“Walimkata mkono wake wa kushooto akiwa amelala na watoto wake wawili kati ya wane, alisema Pillay.

“Mamlaka za Tanzania zina wajibu wa kwanza wa kuwalinda watu wenye ulemavu wa ngozi na kukabiliana na wanao kwepa adhabu ambayo ni sehemu muhimu ya kukomesha uhalifu huo unaowalenga wanyonge hao kwenye jamii.”

No comments: