Wednesday, March 6, 2013

VURUGU ZA IFUNDA SECONDARY:..MKUU WA SHULE ANUSURIKA KUUAWA.KISA NI "BARAGHASIA" DARASANI WANAFUNZI wa Shule ya Sekondari ya Ufundi Ifunda, iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Vijijini, jana walifanya vurugu kubwa shuleni hapo na kutaka kumuua Mkuu wa shule hiyo, Bw. Shaaban Nsute. Katika vurugu hizo ambazo zilianza juzi jioni hadi saa tano usiku, wanafunzi hao ambao walivalia kininja na kuficha sura zao wakiwa na visu mkononi, walivunja vioo vya madirisha shuleni hapo. Wanafunzi hao wanadaiwa kumfuata Bw. Nsute nyumbani kwake lakini alikimbia na kwenda kujificha kwenye shamba la mahindi ambapo wanafunzi hao walimpiga mlinzi wa shule Bw. Yasini Luhala kwa mawe akiwa katika ofisi yake. Akizungumza na Majira jana, Bw. Nsute alisema chanzo cha vurugu hizo ambazo zilidhibitiwa na Jeshi la Polisi ni baada ya mwanafunzi mmoja shuleni hapo kuvaa kofia zinazotumiwa na Waislam (baraghashia). Alisema mlinzi wa shule hiyo, Bw. Luhala alimnyang'anya kofia hiyo ili asiingie nayo darasani kwa sababu si sare ya shule lakini mwanafunzi huyo alichukua uamuzi wa kwenda kuwaita wenzake na kufanya vurugu. Aliongeza kuwa, kutokana na vurugu hizo zaidi ya wanafunzi 30 wamefukuzwa shule na kuwataja baadhi yao kuwa ni Sadi Mwamed, Jamal Hashim na Athuman Ibrahim wanosoma kidato cha tano. Wengine ni Abdulazizi Hussein na Ally Abdallah wanaosoma kidato cha nne. Mwanafunzi aliyenyang'anywa kofia alidai Waislamu katika shule hii wanatengwa, kunyanyaswa na kuzuiwa wasifanye mambo yanayoendana na dini yao. Hawa wanafunzi walikuja nyumbani kwangu usiku na kugonga mlango, nilitoka mlango wa nyuma nikakimbia kwenye shamba la mahindi, mke wangu alifungua mlango na kuwaambia sipona alipowahoji wakamwambia walikuwa wakinihitaji ili niende nao Msikitini kuna kazi muhimu, Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wilayani humo ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya hiyo, Dk Letisia Warioba, alisema tukio hilo limemsikitisha sana. Alilipongeza Jeshi la Polisi kwa kufika mapema eneo la tukio, kutuliza vurugu na kuimarisha ulinzi shuleni hapo hadi asubuhi na kuwataka wanafunzi waliobaki, waendelee na masko kwa kuzingatia taratibu za shule.

WANAFUNZI wa Shule ya Sekondari ya Ufundi Ifunda, iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Vijijini, jana walifanya vurugu kubwa shuleni hapo na kutaka kumuua Mkuu wa shule hiyo, Bw. Shaaban Nsute.

Katika vurugu hizo ambazo zilianza juzi jioni hadi saa tano usiku, wanafunzi hao ambao walivalia kininja na kuficha sura zao wakiwa na visu mkononi, walivunja vioo vya madirisha shuleni hapo.

Wanafunzi hao wanadaiwa kumfuata Bw. Nsute nyumbani kwake lakini alikimbia na kwenda kujificha kwenye shamba la mahindi ambapo wanafunzi hao walimpiga mlinzi wa shule Bw. Yasini Luhala kwa mawe akiwa katika ofisi yake.

Akizungumza na Majira jana, Bw. Nsute alisema chanzo cha vurugu hizo ambazo zilidhibitiwa na Jeshi la Polisi ni baada ya mwanafunzi mmoja shuleni hapo kuvaa kofia zinazotumiwa na Waislam (baraghashia).

Alisema mlinzi wa shule hiyo, Bw. Luhala alimnyang'anya kofia hiyo ili asiingie nayo darasani kwa sababu si sare ya
shule lakini mwanafunzi huyo alichukua uamuzi wa kwenda kuwaita wenzake na kufanya vurugu.

Aliongeza kuwa, kutokana na vurugu hizo zaidi ya wanafunzi 30 wamefukuzwa shule na kuwataja baadhi yao kuwa ni Sadi Mwamed, Jamal Hashim na Athuman Ibrahim wanosoma kidato cha tano. Wengine ni Abdulazizi Hussein na Ally
Abdallah wanaosoma kidato cha nne.

    Mwanafunzi aliyenyang'anywa kofia alidai Waislamu katika shule hii wanatengwa, kunyanyaswa na kuzuiwa wasifanye mambo yanayoendana na dini yao.

    Hawa wanafunzi walikuja nyumbani kwangu usiku na kugonga mlango, nilitoka mlango wa nyuma nikakimbia kwenye shamba la mahindi, mke wangu alifungua mlango na kuwaambia sipona alipowahoji wakamwambia walikuwa wakinihitaji ili niende nao Msikitini kuna kazi muhimu,

Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wilayani humo ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya hiyo, Dk Letisia Warioba,
alisema tukio hilo limemsikitisha sana. Alilipongeza Jeshi la Polisi kwa kufika mapema eneo la tukio, kutuliza vurugu na kuimarisha ulinzi shuleni hapo hadi asubuhi na kuwataka wanafunzi waliobaki, waendelee na masko kwa kuzingatia taratibu za shule.

No comments: