Thursday, May 9, 2013

Mlipuko wa Kanisani Arusha: saba wapelekwa dar kwa matibabu zaidi

 Wagonjwa saba ambao ni majeruhi wa mlipuko wa bomu kwenye kanisa la Joseph Mfanyakazi eneo la Olasiti jijini Arusha wamehamishiwa kwenye Hospitali za Muhimbili na LUgalo jijini Dar es Salaam.

Majeruhi hao wamesafirishwa mchana majira ya saa tisa kwa ndege ya shirika la Hifadhi za taifa (TANAPA) kwenda kuendelea na matibabu zaidi baada ya hali zao kuonekana bado zinahitaji vifaa vyenye uwezo wa hali ya juu.

Miongoni mwa walisafirishwa wapo watoto watatu wakike wawili na wakiume mmoja huu wakina mama walisafirishwa wakiwa wawili na kinababa wawili ambao hali zao bado mbaya licha ya matibabu walikuwa wakiyapata tokea juzi.

Wasamaria wema kutoka makampuni mbali mbali wameendelea kutoa misaada mbali mbali ya hali na mali ikiwemo madawa na vifaa tiba na mablanketi na mashuka,na Magodoro iliviisaidie hospitali za Mt.Meru na St,Elizabeth.

Wakati huo huo wabunge wa jamhuri ya muungano wa Tanzania wamewatembelea wahanga wa bomu na kutembelea kanisa ambalo yalitokea maafa na kujionea hali halisi wakiongozwa na spika wa bunge hilo Anna Makinda.

Miongoni mwa wabunge hao ni Mh.Habibu Mnyaa ambaye alisema kuwa hali kama hiyo imewatia simanzi na kuiomba serekali kuchukuwa tahadhari kubwa kwa matukio kama haya akiongea mbunge wa viti maalumu ccm vijana Catherine Maggige alsema kuwa majeruhi hawa wanatia huruma na kuwa kitendo hicho kilichotokea hakliwezi kuvumilika na kuiomba serekeli kuchukuwa hatua za haraka kukabiliana na wimbi la tukio kama hilo.

Kwa upande wake spika makinda hakuweza kutoa neno lolote bali aliingia kweny Gari teyari kwa safari ya kurudi Dodoma huku akiwa na huzuni kubwa.


Mahmoud Ahmad Arusha

No comments: