Friday, May 3, 2013

FIFA YAWARUDISHA MALINZI NA WAMBURA KUGOMBEA TFF

Kuna taarifa kwamba wagombea wawili, Jamal Malinzi na Michael Wambura wamerudishwa kuwania nafasi walizokuwa wakipigania kuzipata katika uchaguzi mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).

Taarifa kutoka ndani ya TFF zimeeleza, Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) limeandika barua ambayo imeshatua Fifa tayari kuwarejesha Malinzi, Wambura na wengine waliokuwa wanagombea.

Uongozi wa TFF unatarajia kuzungumza muda mfupi ujao kuanzia sasa katika ofisi zake katika eneo la Ilala jijini Dar es Salaam.

Tayari Salehjembe ametega masikio kuhusiana na kitakachotokea na atatutaarifu kama ni hiki kutoka ndani au kutakuwa na mabadiliko.

No comments: