Friday, May 3, 2013

"TANZANIA NI MUHIMU KULIKO CHADEMA.....SIPO TAYARI KUSUSIA MCHAKATO WA KATIBA".....HAYA NI MAJIBU YA PROFESA BEREGU KWA DR SLAA

Kutoka Raia Mwema:

Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha demokrasia na Maendeleo (Chadema), Profesa Mwesiga Beregu, amekataa kata kata wito wa chama chake wa kumtaka ajotoe ndani ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba,huku yeye akiweka msimamo wake wazi kwamba Tanzania ni muhimu zaidi kwake kuliko chama chake hicho.

Habari zilizoppatikana na kuthibitishwa Profesa Baregu, zinasema katibu Mkuu wa chama hicho Dk Wilbroad Slaa, alimwiita msomi ambae ni mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, akimtaka ajitoe. Ndani ya Tume hiyo kwasababu za kisiasa kwa madai kwamba Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimeuteka mchakato huo.

Profesa Beregu anaelezwa kumjibu Dk Slaa kwa kutumia maneno ya kiingereza, "If I am told to choose between my country and my party (Chadema), I will choose my country", akiwa na maana kwamba kama angetakiwa kuchagua kimoja kati ya nchi yake na chama chake cha Chadema, angechagua nchi yake kwanza.

Akizungumza na Raia Mwema juzi Jumatatu jijini Dar es Salaam, Profesa Baregu amekiri kutoa msimamo huo Katibu Mkuu wake Dk Slaa, pamoja na chama chake cha Chadema, akisema viongozi wenzake hao wanapaswa kujishauri mara mbili mbili kabla ya kuchukua uamuzi huo wa kujitoa ikizingatiwa. Kwamba tangu mwanzo chama hicho ndicho kilichoasisi suala zima la Tanzania kuwa na Katiba Mpya tofauti na hii ya sasa.

Itakumbukwa kwamba Chadema, kupitia kwa Mwenyekiti wake, Freeman Mbowe, wakati akiwasilisha hotuba mbadala ya kambi rasmi ya upinzani kwa Ofisi ya Waziri mkuu, alitangaza kujitoa katika mchakato wa mabadiliko ya katiba akitaja sababu kadhaa, zikiwamo za mchakato mzima huo kutekwa na CCM na lakini pia kwamba wajumbe wa Tume hiyo hawana weledi wa kutosha kufanya kazi hiyo.

"Ni kweli niliitwa na katibu Mkuu (Dk Slaa), akaniambia Kamati Kuu ya chama chetu imeazimia kwamba chama hakiridhishwi na mchakato mzima wa kutunga Katiba mpya, na kwa hiyo akaniambia chama kimeagiza nijitoe ndani ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba. Akaniambia Kamati Kuu imeamua mambo mawili; kwanza kijitoe na pili, kikishajitoa kianzishe kampeni ya nchi nzima kuwahamasisha wananchi nao wasusie mchakato huo"anasema Profesa Baregu katika mahojiano maalum na Raia mwema.

Anasema aliomba kujulishwa rasmi maamuzi hayo ya CC kwa maandishi, ili ajue atachukua uamuzi ganilakini hadi anafanya mahojiano na Raia mwema hakuwa amepata majibu huku akisema kwamba kwa maoni yake kama kweli yalikua ni maamuzi ya kikao, basi Kamati Kuu itakuwa ilifanya makosa kufikia uamuzi wa kujitoa bila kumshirikisha.

"Kwanini? Mimi tangu mwanzo kaabisa sikuona kama suala hili la kuandikwa kwa Katiba mpya ni suala la mapambano kwa sababu kubwa moja kwamba Chadema ndiyo mwasisi wa mabadiliko haya ya katiba. Mimi nilikuwa Meneja wa Kampeni za Uchaguzi Mkuu 2010 na nilishiriki kuandika ilani ya uchaguzi, na hili la kutaka Katiba mpya lilikuwemo ndani ya Ilani yetu.

Wakati ule wenzetu (CCM) waliweka msimamo wao wakisema hakuna sababu ya kuwa na katiba mpya, iliyopo inatosha,lakini baadae Serikali ikaona ipo haja ya kuwa na katiba mpya inayokidhi mahitaji ya sasa na yajayo. Muswada ukapelekwa Bungeni, wabunge wa upinzani wakasusa na kutoka nje. Chadema tukapewa fursa ya kwenda Ikulu kuonana na Rais kwa siku mbili mfululizo na karibu mapendekezo yetu yote yakakubaliwa."

"Muswada ukarudishwa Bungeni upya, sheria ikafaniwa marekebisho na kukubalika na wabunge wa kambi ya upinzani. Sasa leo hii, wabunge wale wale waliokubali, wanataka kukataa mchakato wa katiba unaoendeshwa kwa mujibu wa sheria waliyoipitisha wao wenyewe....kwa maoni yangu, hadi sasa sijaona matatizo ya mchakato., yawe ya maandishi au ya malengo ya kisheria. Kama ningekuwa nimeona tatizo nisingekuwa humu, ningejitoa, Tunatengeneza Katiba yetu Watanzania wote, si Katiba ya Chama fulani...

"Lakini pia, chadema tulipokutana na Rais (Jakaya Kikwete), alitushauri na tukakubaliana naye, twende hatua kwa hatu. Itungwe sheria yenyewe kwanza, halafu iundwe tume, baada ya hapo mambo mengine yaendelee kujadiliwa...(Angu wakati huo hadi sasa nadhani sisikama Tumetunafanya vizuri ikilinganishwa na wenzetu wa huko nje walioandika upya Katiba yao.

"Mchakato unaofuata sasa ni wa kuundwa kwa bunge Maalumu la katiba, hatua hii nayo Wananchi wanetakiwa wajiandae kutoa maoni yao juu ua muundo wa. Bunge hilo. Ushauri wangu kwa Chadema., naomba chama chetu kikae mkao wa kujenga nchi yetu, si. Mkao wa kuibomoam Kama Chama tukae na Watanzania kujenga Katiba yetu mpya kwa ajili ya Watanzania na Tanzania yetu hii kwasababu fursa hii haitakuja tena karibuni labda baada ya miaka 50 ijayo....kuzira, kujitoa, nasema Watanzania hawatatuelewa"

Kaifafanua msimamo wake alioutoa kwa Dk Slaa kwamba kama angeambiwa achague kati ya ncchi yake na chama chake, angechagua nchi kwanza, Profesa Baregu anasema "Ndio, chama kinaundwa kinapita, lakini Tanzania kama nchi itaendelea kuwepo daima. Ushauri wangu kwa Chadema ni kwambakwa kuwa sisi tulishajiweka katika kusimamia mchakato wa Katiba mpya, tusijiharibie kwa kuvuruga mchakato huu"

Akizungumzia kauli ya Mbowe katika hotuba yake bungeni kwamba Tume ya Mabadiliko ya Katiba haina watu weledi, Profesa Baregu anasema "Sisemi katika hili Chadema imekurupuka, nasema ijishauri upya, sijui ni weledi wa aina gani wanaousema, lakini naamini Tume yaMabadiliko ya Katiba imejaa watu weledi watupu, imejaa watu waadilifu na wasiokuwa na matope yeyote...,ndiyo maana tangu iundwe, hakuna Mtanzania yeyote ambae ameiita Tume hii kwamba ni genge jingine la mafisadi.

"Sitaki kuwasemea wajumbe wanzangu juu ya weledi wao, lakini mimi mwenyewe tu mbali na elimu yangu, lakini pia nimetumika katika Tume ya Month Ibrahim inayotathimini utawala bora wa marais wa Afrika kwa muhula mmoja, mtu huwezi huwezi kuwa katika tume hiyo kama huna weledi wa kutosha"

Dk Slaa alipotafutwa jana Jumanne,ili pamoja na mambo mengine alezee hatua hiyo ya Profesa Baregu kukataa kujiuzulu akiweka wazi kwamba hadi sasa hajaona tatizo lolote kubwa ndani ya Tume hiyo linaloweza kumshawishi akubaliane na msimamo wa chama chake, na msisitizo wake huo wa kuweka maslahi ya nchi kwanza mbele kuliko chama chake alisema "Saa hizi niko kwenye kikao, pole baba"

No comments: