Friday, May 24, 2013

TANZANIA,KENYA ZAVUTANA JUU YA VIJANA WALIOUWAWA NAROK

                                            Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha Liberatus Sabas

MIILI  mitatu ya watanzania wa jamii ya Kisonjo waliouwawa katika eneo la Narok wilayani Kajiado nchini Kenya imeingia katika sura mpya mara baada ya Serikali ya Tanzania kushindwa kuirejesha nchini miili hiyo huku serikali ya Kenya ikidai kuwa hawakuwa watanzania

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha Liberatus Sabas alisema kuwa tayari mtu mmoja ambaye ni askari polisi anashikiliwa na jeshi hilo kwa uchunguzi zaidi ingawaje alisema kwa sasa jina la askari huyo linahifadhiwa kwa ajili ya  upelelezi

Sabas alisema kuwa wanamshikilia askari huyo kwa kosa la upotevu wa silaha ambayo inasadikiwa kuwa ilitumika katika tukio uhalifu linalohusishwa na mauji ya vijana hao watatu wa Kitanzania nchini Kenya.

Kuhusu Marehemu hao, kamanda amesema kuwa Serikali ya Kenya kupitia Jeshi lake la polisi ndio wanajukumu la kurejesha  Miili yao hapa nchini .


Awali Msemaji wa familia tatu za marehemu hao,Pasto Webo alidai kuwa askari wa kituo cha polisi Loliondo waliwatoza kiasi Milioni mbili na nusu kwa ikiwa kama gharama za kuwasafirisha marehemu kutoka kenya kwa gari la Polisi kwa kiwango cha shilingi laki nane kwa kila mwili mmoja.

Lakini Kamanda wa Polisi alisema kuwa Jeshi hilo halina utaratibu wa kusafirisha marehemu na kwamba anafuatilia madai hayo na itakapobainika kuwa ni kweli watachukuliwa hatua kali za kisheria.

Kuhusu kuhusika kwa polisi wa loliondo na kupotea kwa vijana wao watatu msemaji wa familia hizo tatu alidai kuwa May tatu mtoto wake ambaye ni Tibiti webo alikuja nyumbani kwake akiwa na askari polisi ambaye anajulikana kwa jina la Lazaro ambapo walikula chakula na walipoondoka kwa pamoja kijana huyo hakuonekana tena.

Pia alidai inasemekana kuwa kijana huyo alimpitia  rafiki yake ambaye amejulikana kwa jina la Kadogo anna ambapo tangu alipoondoka  tarehe tatu mwezi huu hawakuonekana tena  mpaka  hivi karibuni polisi walipowaletea ripoti pamoja na picha kuwa vijana wao wameuwawa vibaya Narok

“Tulipotazama hizo picha tuliweza kuwatambua vijana wetu wawili  lakini pia alikuwepo mwingine wa tatu ambaye tunadhani kuwa anatokea kijiji cha jirani”

Inadaiwa kuwa polisi waliwaeleza kuwa vijana wao waliuwawa katika tukio la ujambazi  katika eneo la Narrok  ambapo ilidaiwa kuwa waliwavamia wafanyabiashara kwa ajili ya kuwapora fedha lakini wakauwawa na wananchi wenye hasira kali

Katika tukio hilo vijana hao walikutwa na silaha ambayo inaaminika kuwa walipewa na askari wa kituo cha polisi cha loliondo.

Akizungumza kwa njia ya simu kutoka Dar es salam balozi wa Kenya Nchini Tanzania ,Mutinda Mutiso alidai kuwa vijana waliouwa sio watanzania bali ni wa Kenya huku akiongeza kuwa tukio hilo lilitokea wakati yeye akiwa nchini humo.

No comments: