Monday, June 3, 2013

GARI LA WEMA NYANG’ANYANG’A

GARI la Wema Isaac Sepetu ‘Beautiful Onyinye’ limepata ajali na kuwa nyang’anyang’a huku dereva aliyekuwa akiliendesha akiumia vibaya.


Gari la Wema kwa ndani baada ya ajali hiyo.

Habari zilisema kuwa ajali hiyo ilitokea maeneo ya Morocco, Kinondoni jijini Dar, wikiendi iliyopita ambapo dereva huyo ambaye inadaiwa ni ‘jamaa wa Wema’ aliyetajwa kwa jina moja la Robby aliumia mguu wa kushoto na taya hivyo kukimbizwa hospitali (jina halikupatikana mara moja).


Gar la Wema baada ya ajali.

Gari la Miss Tanzania huyo wa mwaka 2006/07 lililopata ajali ni lile dogo aina ya Toyota Mark X lenye namba za usajili T 426 CHM ambalo liliharibika vibaya sehemu ya mbele huku vibaka wakidaiwa kutumia nafasi hiyo ‘kulisafisha’ vitu ndani.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, mwanadada Wema alitupia picha za ajali hiyo huku akijitetea kuwa aliyepata ajali na gari hilo ni mfanyakazi wa kampuni yake ya Endeless Fame.

Robby akiwa na majeraha baada ya ajali.

Kwa mujibu wa meneja wa staa huyo wa filamu, Martin Kadinda, jamaa huyo alikutana na ajali alipokuwa akirejea kwake akitokea nyumbani kwa Wema na kwamba anaendelea vizuri baada ya kupatiwa matibabu.

No comments: