Thursday, February 7, 2013

Askofu Leizer wa KKT amefariki dunia

                            Askofu wa Kanisala KKKT Thomas Leizer enzi za uhai wake

ASKOFU  wa lKanisa la Kiinjili la Kirutheli Tanzania ( KKKT) Dayosisi ya Kaskazini Kati, Thomas Laizer amefariki dunia alasiri ya leo katika Hospitali ya Rufaa ya Selelian ya Mjini Arusha.

Askofu Leizer amefikwa na mauti ikiwa ni siku moja baada ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda kumjulia hali hospitalini hapo.Taarifa zilizolifikia hivi punde zinadai kwamba Askofu Laizer alilazwa Hospitalini hapo kwa zaidi ya mwezi mmoja, na hakuna Daktari wala ndugu aliyekuwa tayari kusema ugonjwa uliokuwa ukimsumbua.

Waziri Mkuu alifika hospitalini hapo jana saa saa 9 alasiri na kukaa zaidi ya nusu saa, huku waandishi wa habari wakizuiliwa kuingia katika chumba alimolazwa cha wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalumu wa Madaktari (ICU).

Hata hivyo, baada ya kutoka katika chumba hicho kama ilivyo ada ya viongozi kuzungumzia hali ya mgonjwa, Pinda hakuzungumza na waandishi wa habari na kulikuwa na ulinzi mkali ambapo pia waandishi wa habari walizuiliwa kuzungumza na mgonjwa huyo.

Kabla ya Waziri Mkuu kufika katika hospitali hiyo na kumjulia ali taarifa zilizowahi nkutolewa na ndugu pamoja na watu wa karibu ikiwemo uongozi wa hospitali hiyo ilidai kwamba Askofu Laizer alihamishiwa katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC ya Moshi Mkoani Kilimanjaro, baada ya watu wengi kumiminika katika Hospitali ya Selian kutaka kumjulia hali.

No comments: