Thursday, February 7, 2013

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete azindua vitambulisho vya taifa

 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akibonyesha kitufe kuashiaria kuzindua rasmi mfumo wa usajili na utambuzi wa watu na utoaji wa vitambulisho vya taifa uliofnyika katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam leo.Watatu kushoto ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi Dkt.Emmanuel Nchimbi, kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa NIDA Bwana Mwaimu na kulia nia Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Bwan Said Meck Sadik.
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam wakiangalia bango lenye kitambulisho cha  taifa cha Rais Kikwete muda mfupi baada ya Rais Kikwete kuzindua mfumo wa Usajili na utambuzi wa watu na utoaji wa vitambulisho vya taifa uliofanyika katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam leo.Kushoto ni Waziri wa Mambo ya  Ndani ya Nchi Dkt.Emmanuel Nchimbi

 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Dkt.Emmanuel Nchimbi akimkabidhi Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete kitambukisho cha Taifa katika hafla ilkiyofanyika katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam leo.
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Dkt.Emmanuel Nchimbi akimkabidhi mke wa Rais Mama Salma Kikwete kitambulisho chake cha Taifa katika viwanja vya Karimjee leo huku Rais Kikwete akishuhudia.Kushot o Mkurugenzi Mkuu wa NIDA Bwana Mwaimu.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi Rais Mstaafu awamu ya pili Mzee Ali Hassan Mwinyi kitambulisho chake cha taifa katika viwanja vya Karimjee leo.

No comments: