Wednesday, December 31, 2014

Kanye West na Kim Kadarshian wamenunua nyumba mpya


 Ratiba za mastaa wengi walio katika uhusiano wa kimapenzi huwa zinawafanya wanakuwa busy na kushindwa kupata time ya kuspend pamoja, Kim Kardashian na Kanye West ni moja ya mastaa ambao wao pia ratiba yao huwa ngumu kupata muda wa kukaa pamoja.
 Kim yuko busy na TV show na deal zake za mitindo lakini ratiba yake haimfanyi awe busy kama ilivyo kwa Kanye ambaye amekuwa akizunguka kwa ajili ya show na pia kurekodi nje ya Marekani.

Story ya mwisho kusikika kuhusu mastaa hao ni ile ambayo imetoka siku moja iliyopita, wamenunua nyumba ya jirani yao yenye thamani ya dola mil.3 maeneo ya Los Angeles ambapo mkakati walio nao ni kuikarabati kwa kuweka vitu kadhaa ikiwemo Studio ya kisasa.
Kwenye nyumba hiyo pia kutakuwa na uwanja wa basketball, sehemu ya kuangalia filamu, sehemu ya michezo, chumba cha massage na eneo la kufikia wageni, studio itakayokuwepo hapo huenda ikasaidia kumfanya Kanye apate muda mwingi kidogo wa kukaa nyumbani tofauti na ilivyo sasa.

No comments: