Wednesday, December 31, 2014

Zitto Kabwe kuhusu Serikali kutekeleza maazimio yaliyotolewa na Bunge…

                                                                      Zitto-Kabwe1

Mbunge wa Zitto Kabwe leo amewahutubia Wananchi wa Mtwara kupitia mkutano ulioitishwa na chama cha Wananchi CUF na kutoa ufafanuzi juu ya sakata la account ya Tegeta Escrow.

Akizungumzia sakata hilo Zitto Kabwe amesema kuwa baadhi ya viongozi waliohusika na sakata hilo ambao mpaka hivi sasa hawajachukuliwa hatua yoyote lazima wachukuliwe kwa kuwa serikali haiwezi kupingana na maazimio ya bunge.

“ Utekelezaji wa maamuzi ya Bunge hauna mjadala… sisi kama Wabunge wa Kambi ya Upinzani mwezi January kazi ya kwanza ni kupokea taarifa ya utekelezaji wa maamuzi ya Bunge… Tunachokitaka kila mtu aliyehusika kwenye Escrow ni lazima awajibike…“– Zitto Kabwe.

Sisi lazima tuutumie mwaka 2015 kama mwaka wa uwajibishaji, mwaka wa kuwajibishana… safari hii mmewawajibisha kwenye Seikali za Mitaa, hongereni sana, tunaenda kuwawajibisha kwenye Serikali kuu sasa…”– Zitto Kabwe.

No comments: