Wednesday, July 4, 2012

HUYU NDIO MISS DAR INDIAN OCEAN 2012, NA HII NI SEHEMU YA MAGUMU ALIYOYAPITIA.



                                                     Diana Hussein Miss Dar Indian Ocean 2012.
Kuna asilimia kubwa ya mastaa au watu maarufu unaowapenda au kuwafaham kupitia  TV, Magazeti, radio na internet lakini umaarufu walionao haujaja kirahisi.

Stori nyingi sana za mastaa kusikia alikoanzia, na ni mbali wengi sana wametoa jasho debe kufikia walipo mtu kama Sean Kingston ambae aliwahi kuja bongo kwenye KTMA aliwahi kufanya kazi ya kukata nyasi kwenye garden za watasha ili mwisho wa day zipatikane dola kwa ajili ya kula, nakumbuka mwaka jana aliandika kwenye twitter kwamba kazi ya kuwa msimamizi wa garnen aliichukia sana.

Tukirudi home bongo, wako mastaa kibao wameanza kwa kusota sana… au kupitia kwenye mambo magumu ya maisha pia akiwemo binti mrembo ambae juzi juzi ndio alivishwa taji la miss Dar Indian ocean Diana Hussein,  ni mrembo lakini mwenye makovu mengi ya kimaisha yasioyoonekana kwenye ngozi yake nzuri, ameanza kufanya kazi miaka mitatu iliyopita akiwa na umri wa miaka 17 tu kazi ambazo hakuzipenda kabisa lakini alifanya hivyo kwa sababu ya maisha.

Baada ya kukosa ada ya kuendelea na masomo ya sekondari ilibidi Diana aje Dar akitokea Tanga na kuanza kazi yake ya kwanza ya kuajiriwa kwenye duka la dawa, aliifanya hiyo kazi kwa mwaka mmoja na baadae huku akiwa na machungu ya kuisaidia familia yake kiuwezo aliamua kutafuta kibarua kingine na akafanikiwa kuwa mkaribisha wageni kwenye kampuni moja Dar es salaam, kazi zote hizo alizifanya lakini hakuwahi kuzipenda kabisa.

Japo bado hajatimiza ndoto zake lakini amefikia kwenye hatua ya kuridhisha baada ya kuacha kazi za kuajiriwa mwaka huu na kuanzisha biashara yake ya kuuza vitu vya warembo wenzake, kama mikufu, perfume na vingine…. huku mawazo yake yakimpa msukumo wa kufanya vizuri zaidi kwenye mashindano yanayofata ya juu zaidi.

No comments: