Wednesday, July 4, 2012

HIVI UMEMSIKIA KIPA SHABAN KADO ALICHOSEMA KUHUSU KURUDISHWA MTIBWA? UNAYAJUA MAONI YAKE KUHUSU KIPA MPYA YANGA ALIETOKA SIMBA?

                                           Kipa Shaban Kado kushoto mwenye jezi nyeusi
Kwa long time kidogo stori zimekua zikiandikwa kwenye magazeti, Radio na Tv kuhusu kipa wa Yanga Shaban Kado ambae club hiyo imetangaza kumrudisha kucheza kwa mkopo Mtibwa Sugar hivyo ikasajili kipa mwingine mpya ambae ni Bartez kutoka Simba.

Amesema “hizo taarifa nilianza kuzisikia kwenye vyombo vya habari bila mimi mwenyewe kuambiwa na uongozi lakini baadae nikafanya mawasiliano na boss wangu na sasa tuko kwenye mikakati ambayo ikikamilika ndio itajulikana Kado anakwenda wapi, inaweza kuwa sio Mtibwa”

Kuhusu Kurudi Mtibwa Kado amesema “kwa makubaliano ikitokea hivyo ninaweza kurudi kwa sababu ni timu yangu iliyonifanya kila mtu anasikia kuhusu Kado, sitakataa kurudi Mtibwa ila itategemea itahitajika nirudi vipi na kuhusu ishu ya mimi kuondolewa Yanga kuna sababu tu nazifaham ambazo baadae zitakuja kujulikana”

Kuhusu stori za kurudishwa Mtibwa kwa sababu kiwango chake cha uchezaji kimeshuka akiwa Yanga, Kado amesema  “katika mechi zote za Yanga nimepoteza mechi mbili au tatu, sasa utaniambiaje kiwango kimeshuka wakati kupoteza mechi ni kitu cha kawaida tu”

Kado ambae ni mmoja kati  ya wachezaji wa kibongo wanaotumia sana mtandao wa kijamii wa facebook amekubali kuzungumzia ishu za yeye kuhamia kwenye club nyingine ikiwemoa Simba ambayo inadaiwa kumuita kwa ajili ya kumpa mkataba.

Katika sentensi nyingine Kado amesema mpaka sasa hayuko tayari kuzungumza ni timu gani atakayokwenda kuichezea baada ya Yanga lakini amethibitisha kwamba kuna uwezekano akarudi Mtibwa au timu nyingine yoyote.

 Chanzo: millardayo.com

No comments: