Thursday, July 5, 2012

ILICHOSEMA MOI KUHUSU MADAKTARI WAKE BINGWA.

Taasisi ya mifupa Muhimbili MOI imesema Madaktari bingwa 18 wa taasisi hiyo wanaendelea na kazi yao kama kawaida na hawajihusishi na mgomo kama inavyoripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari huku ikiendelea kutoa huduma za wagonjwa wa dharura na wale wa kawaida.

Akitolea ufafanuzi kuhusu tamko lililotolewa na jumuiya ya Madaktari kwamba Madaktari bingwa wote wamejiunga kwenye mgomo huo, mwenyekiti wa bodi ya Udhamini ya MOI Balozi Mstaafu Charles Mutalemwa amesema tangu kuanza kwa mgomo huo june 23 mwaka huu Taasisi hiyo imeendelea kuhudumia wagonjwa licha ya kugoma kwa madaktari walio kwenye mafunzo katika hospitali ya taifa Muhimbili.

Kwenye sentensi nyingine, Mutalemwa ametaka vyombo vya habari kutochanganya Taasisi ya mifupa MOI na hospitali ya taifa Muhimbili kwa sababu kila moja ni taasisi inayojitegemea na kila moja ina bodi ya maamuzi yake ingawa wanashirikiana kikazi.Thanx http://millardayo.com/

No comments: