Saturday, August 4, 2012

MAMA MARIA NYERERE AKABIDHI MATREKTA KUMI KWA WAKULIMA WA KATA YA KWADELO, KONDOA

 Mjane wa Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere, Maria Nyerere, akimkaribisha, diwani wa Kata ya Kwadelo, wilaya ya KLondoa mkoa wa Dodoma, Alhaj Omar Kariati, wakati diwani huyo na ujumbe wake wa wakulima kumi, walipofika nyumbani kwa Mama Nyerere kwa ajili ya kukabidhiwa trekta kumi kwa wakulima hao, katika sherehe iliyofanyika nyumbani kwa Mama Maria Nyerere, Msasani jijini Dar es Salaam, leo.
                           Kariati akizungumza neno la kufungua shughuli. Kulia ni Mama Nyerere
Kisha Kariati akamkabidhi zawadi ya Kitenge Mama Nyerere kama shukurani ya wananchi wa Kwadelo kujengewa kisima cha maji na baba wa Taifa Mwalimu mwaka 1961 ambacho hadi sasa kipo.
                         Halafu akamkabidhi mkoba wa safari kama akitaka kwenda Butiama
Mama Nyerere akapata fursa ya kuzungumza mambo mbalimbali kabla ya kukabidhi trekta kwa wakulima hao, ambao pichani wamekaa kushoto.
       Mama Maria Nyerere na Kariati wakaongozana na wakulima kwenda eneo la makabidhiano ya trekta
                     "Trekta zenyewe ndiyo hizi" akasema Kariati kumwambia Mama maria Nyerere
 Mama Maria akimkabidhia funguo za trekta moja kati ya kumi aliyokabidhi, mmoja wa wakulima hao Sheikh Hamis Haji ambaye pia ni Sheikh wa Kata ya Kwadelo.
                       Baadha ya Sheikh akamkabidhi pia mkulima Maulidi Msema funguo za trekta
                     Baada ya Mama Nyerere kukabidhi trekta kumi, Kariati akamshukuru
     Kisha Mama Nyerere na diwani Kariati na Wakulima wakapigwa picha ya pamoja kuhitimisha shughuli

No comments: