Saturday, August 4, 2012

ROMA APATA AJALI MBAYA NA GARI LEO,

                                                            Gari Lilivyoharibika
 Msanii wa Bongo fleva Roma Mkatoliki amepata ajali mbaya ya gari Morogoro road ambapo kwa mujibu wa Roma ni kwamba tairi la mbele lilipopasuka na gari likaacha njia na kugongana uso kwa uso na fuso ambalo lilikuwa upande wa pili na gari hilo dogo alilokuwa akiendesha na kurudi lilipotokea.

Roma amesema kwamba anaelekea hospital kwa check up zaidi ila aliokuwa nao kwenye gari hakuna aliyeumia wote ni wazima.
Roma amepata ajali hii leo ikiwa ni siku 18 tu toka msanii mwingine wa bongofleva Chege kupata ajali ya gari yake kwa kumgonga mtu wa pikipiki alieingia barabarani ghafla na kusababisha gari kuharibika

No comments: