Wednesday, October 17, 2012

RAIS SHEIN AWAAPISHA VIONGOZI ALIOWATEUA KARIBUNI

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohd Shein akimuapisha Bi Shawana Bukheti Hassan kuwa Mjumbe wa Baraza la Mapinduzi na Waziri asiekuwa na Wizara Maalum katika hafla iliofanyika Ikulu Mjini Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohd Shein akiwa katika Picha ya Pamoja na Mawaziri na Manaibu Makatibu wakuu aliowaapisha leo Ikulu Mjini Zanzibar.


 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Ali Mohamed Shein leo amewaapisha Mawaziri na Manaibu Makatibu Wakuu aliowateua hivi karibuni

 Walioapishwa ni Mjumbe wa Baraza la Mapinduzi na Waziri asiyekuwa na Waizara maalum Shawana Bukheti Hassan,Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mohamed Said na Naibu Waziri wa Kilimo na Mali Asili Mtumwa Kheir Mbaraka

Wengine walioapishwa na Dkt.Shein ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano Taahir Mohamed Khamis,Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi,Makazi,Maji na Nishati Mustafa Aboud Jumbe.

 Pia aliwaapisha Naibu Katibu Mkuu katika Ofisi ya Rais Fedha,Uchumi na Mipango ya Maendeleo Juma Ameir na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi anayeshighulikia Idara Maalum za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar CDR Julius Nalimy Maziku.

 Miongoni mwa viongozi ambao walitarajiwa kuapishwa leo na hawakuwepo ni Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi,Makazi,Maji na Nishati Ali Khalil Mirza na Katibu Mkuu Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano Dkt Juma Malik Akili

 Shuguli hiyo ambayo ilifanyika Ikulu mjini Zanzibar ilihudhuriwa na Makamo wa Kwanza wa Rais Maalim Seif Shariff Hamad,Makamu wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Idd,Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Pandu Ameir Kificho, Mawaziri mbalimbali,Washauri wa Rais, Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Maalim Abdalla Mwinyi Khamis,Kadhi Mkuu wa Zanzibar Khamis Haji,Maofisa wa ngazi mbalimbali za Serikali, pamoja na baadhi ya Wakuu wa Vikosi vya SMZ.


Na Maelezo Zanzibar

No comments: