Wednesday, October 17, 2012

Sheikh Farid wa Uamsho 'atekwa nyara' visiwani Zanzibar



Habari zilizogaaa kila kona sasa hivi unguja kuwa Sheikh Farid wa Uamsho ametekwa na watu wasiojulikana na hadi sasa hajulikani yuko wapi.

Mengi tuthabarishana. Ila kwa sasa hali ni tee maana watu washaqnza kujikusanya kila pahala.

Uhalisia wa kinachoendelea kama ifuatavyo:

    - Kwa mujibu wa Katibu wake, Abdallah Said Ally, amesema alikuwa na dereva wake maeneo ya Michenzani akitokea nyumbani kwake Mbuyuni, ndipo akakutana na gari moja ambalo dereva halifahamu na akashuka mwenyewe kwenye gari lake na kuingia katika hilo gari na kuanzia hapo hadi sasa hajulikani alipo.
    - Katibu huyo wa Uamsho na wenzake wamekuwa katika juhudi za kutuliza jazba za wafuasi wao na sasa wanawasiliana na polisi kujua alipo kiongozi wao.
    - Sheikh Farid 'amepotea' muda ule ule ambao inadaiwa mwenzake (Sheikh Ponda) alikamatwa (saa 5 usiku wa kuamkia leo). Juu ya sakata la Sheikh Ponda fuatilia - Sheikh Ponda akamatwa Dar!
    - Hata hivyo, wananchi wa hapa Zanzibar wanasema polisi, UAMSHO na serikali wangesubiri wanafunzi wamalize mitihani ya Form 4 kabla ya wao kuanza malumbano yao!

Chanzo Jamiiforum.

No comments: