Saturday, January 5, 2013

Mama Bilal Mgeni Rasmi Tambaza

 Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Asha Bilal, akisoma hotuba yake wakati alipokuwa mgeni rasmi kwenye Mahafali ya Kidato cha Sita kwa Jumuiya ya Wanafunzi wa Kiislamu wa Shule ya Sekondari ya Tambaza. Mahafali hayo yamefanyika leo Januari 05, 2013 katika shule hiyo ya Tambaza jijini Dar es Salaam. Katika hotuba yake Mama Asha amewahasa vijana hususan wanafunzi hao waliohitimu masomo kutokukubali kutumika na watu wenye maslahi binafsi na kujikuta wakisababisha uvunjifu wa amani. Aidha amewataka kutojihusisha na makundi yanayochochea uvunjifu wa amani bila kujitambua wafanyalo, badala yake amewaomba kuwa wakipima kila wanaloambiwa kuwa linamaslahi na dini yao ama maslahi kwa jamii na taifa kwa ujumla.

Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Asha Bilal, akimkabidhi zawadi mhitimu wa Kidato cha Sita, Zuhura Azmin, kwa kuwa mmoja kati ya waliofanikisha sherehe za mahafali ya Kidato cha Sita kwa Jumuiya ya Wanafunzi wa Kiislamu wa Shule ya Sekondari ya Tambaza

No comments: