Monday, April 15, 2013

MBOWE AMKAANGA ZITO KABWE...ADAI KUWA LWAKATARE HATOFUKUZWA CHADEMA HATA KAMA NI GAIDI

 Katika hali ya kushitua,Mh.Mbowe akiongea na wanachama wa chadema leo Ubungo plaza amemkaanga  Zitto  kabwe  na  kudai  kuwa  chadema  haiko  tayari  kumtimua  Lwakatare  katika  chama  hata  kama  ni  gaidi....

"Eti nashangaa kuna watu wanataka CHADEMA kimuache Lwakatare na kumsimamisha uongozi kwa uzushi uliopandikizwa na CCM, Hilo halitafanyika"- alisema Mbowe.

IKUMBUKWE siku chache zilizopita naibu katibu Mkuu wa CHADEMA Mh. Zitto Kabwe alitoa mapendekezo ya kuomba Mshitakiwa mkuu kwenye kesi ya Ugaidi ambaye ni Ndugu Lwakatare aliyekuwa mkuu wa usalama wa chadema awajibike kisiasa...
 Kuwajibika kisiasa ni pamoja na kuachia ngazi ya ukurugenzi wa usalama ili kupisha uchunguzi salama na kukiacha chama salama.


Katika  barua  yake  kwa  chama  chake,Zitto  Kabwe alikitaka  chama kijichunguze  kuhusu  shutuma hizi  za  ugaidi zinazokikabili huku Lwakatare akiwa nje ya ulingo wa viongozi waandamizi wa chadema.

Hata hivyo katika hali ya kustaabisha barua ya zitto ilivuja na  kusambaa  mitandaoni wakati Zitto Kabwe anadai   kuwa ilikuwa ni barua ya siri kati yake na ofisi ya katibu mkuu wa chadema....

Kauli ya Mbowe  leo  hii  kumkana zitto Kbwe mbele ya wanachama wa  inaleta sura mbili  ndani  ya  chama  hicho  cha  upinzani:

Mosi:Barua ya mapendekezo ya Zitto ilivujishwa kwa maksudi kama njia ya kumpinga zitto....

Pili: Kauli ya Mbowe ya leo inamkingia kifua katibu mkuu kutowajibika kwa kuvujisha barua kwa sababu barua haikubebe ujumbe wenye maana kwa chama na Lwaktare
Tatu: Madai  ya UGAIDI dhidi  ya  Lwakatare  na  Chadema  kwa  ujumla  ni  ya  kweli  ,hivyo  chama  kinajukumu  la  kumlinda  Lwakatare  ili  kuuficha  ukweli  usijulikana

No comments: