Monday, April 15, 2013

ZITTO KABWE AIKANA NAMBA YAKE YA SIMU LIVE BAADA YA CHADEMA WENZAKE KUDAI NI GAIDI NA ACHUNGUZWE

 Sasa  nashawishika  kuamini  kuwa  CHADEMA  wana  lao  juu  ya  mipango  ya  kigaidi...

Jana  Mabere  marando  alitoa  tamko refu  sana   lenye  namba  za  simu  kibao  za  watu  mashuhuri  akitaka  mahakama  ichunguze  simu  zao  ikiwemo  ya  Zitto  Kabwe.....

SWALI  LA  KUJIULIZA:

-Kwanini Mabere Marando anatoa tamko muhimu kama hili bila kuhussisha viongozi wa juu kama Zitto?

-Matamko ya nini wakati kesi iko mahakamani?

-Kwanini chadema inaendelea kulizungumzia hili swala nje ya mahakama huku wanaharakati wa chadema kama Mwanakijiji wakiwa wameshaanzisha harakati za kutaka kesi ifutwe kwa swala kuzungumziwa nje ya mahakama?

 HUU  NI  UJUMBE  WA  ZITTO  AKIKANUSHA  KUHUSIKA  NA  UGAIDI

 ( HAPA  AMEANZA  KWA  KUNUKUU  SEHEMU  YA RIPOTI  YA MABERE:)


Ndugu waandishi wa habari;
Pili, nitakwenda mahakamani kuwasilisha ombi maalum la kuomba amri ya mahakama kuagiza makampuni ya simu za mkononi kuwasilisha mahakamani statement za simu za watu kumi (10) ili kusaidia mahakama kutenda haki na jamii kujua ukweli wa mambo haya.

Watu ambao nitaomba mahakama itoe amri ya kuletwa taarifa zao simu na meseji (sms) ni Naibu Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa nchini (TISS), Jack Zoka, anayetumia simu Na. 255756809535, Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mwigulu Lameck Nchemba....

HUU  NDO  UTETEZI  WAKE


Namba hiyo iliyotajwa katika TAMKO imewahi kuwa namba yangu ya Simu. Namba hii nimeacha kuitumia toka mwezi Juni/Julai mwaka 2012.

Hata hivyo namba hii bado inaonekana kwenye business card yangu na kwenye email zangu sehemu ya anuani. Namba hii haijawahi kuwa ya Zoka. Imewahi kuwa ya Zitto Zuberi Kabwe peke yake. Namba hii haitumiki toka katikati ya mwaka 2012.

Mambo mawili  muhimu:ama namba hii imewekwa kwa bahati mbaya kwenye tamko tajwa au imewekwa makusudi kwa sababu maalumu zenye lengo la kutoa ujumbe fulani kwa watu.

Kwa namna namba hii ilivyochomekwa kwenye tamko hili  ni dhahiri kuna juhudi za kunihusisha na upuuzi huu wa ugaidi na unyama dhidi ya binaadamu.

Napenda kusisitiza kwamba, sihusiki kwa namna yeyote ile katika kuwaza, kupanga au kutekeleza mipango yeyote ya kudhuru mtu ama kwa njia za kigaidi au za kijinai.

Sihusiki kwa namna yeyote ile kupanga mpango wowote ule wenye lengo la kuhusisha chama changu na vitendo vyovyote vya kigaidi au kudhuru mtu yeyote yule.

Juhudi zozote zinazofanywa na maadui wa chama changu za kunihusisha na mambo haya zitashindwa kwani siku zote ukweli huwa bayana.

Napenda kuweka wazi kwamba Mhariri wa Mwananchi ndugu Dennis Msacky ni rafiki yangu wa karibu sana.

Ninaamini kabisa kwamba katika suala hili Dennis Msacky ni victim. Juhudi zozote zile za kutaka kumgeuza 'victim' kuwa mtuhumiwa lazima zitashindwa tu kwani siku zote HAKI hutamalaki.

Mtu yeyote anayetaka kutumia urafiki wangu na Dennis Msacky kutaka kujifurahisha kisiasa ajue kuwa furaha yake hiyo itakuwa ni ya muda mfupi sana maana ukweli ukidhihirika atapata aibu kubwa sana.

Ni muhimu sasa mambo haya tuiachie mahakama itende haki.

No comments: