Saturday, April 13, 2013

PADRI ALIYEOA KWA SIRI AFUNGWA JELA MIEZI 6

KUSHOTO: Padri William akimbusu mkewe, Beverley. KULIA: Kanisa la Mt. Clara ambamo Padri huyo alibambwa akifanya uchavu wake kwa binti wa miaka 17.

Padri mmoja wa kanisa Katoliki ambaye alifunga ndoa kwa siri amehukumiwa kifungo cha miezi sita jela jana kwa kumsumbua msichana mdogo kwa kile jaji alichoelezea 'uvunjifu mkubwa wa uaminifu'.

William Finnegan, akifahamika kama 'Fadha Bill', alimpapasa binti huyo mwenye miaka 17 chini na kulazimisha kumbusu kwa nguvu katika Kanisa Katoliki la Mt Clara mjini Bradford siku ya Jumapili ya Pasaka mwaka jana.

Jaji Roger Thomas alisema kwamba Padri huyo mwenye miaka 60, alikiri wakati wa kesi hiyo kwamba alifunga ndoa kwa siri miaka 14 iliyopita.
Pia alitumia maneno makali kwa wanaparokia wa Finnegan ambao walikuwa upande wake licha ya mashitaka hayo, akisema: "Pengine baadhi yao wanaweza kuamini kesho jua litachomoza magharibi kesho kama akisema hivyo."

Thomas aliongeza: "Kwangu inaonekana hawezi kuinua sura yake kwa haya aliyofanya.
"Sifahamu nini kilichomsukuma lakini pengine ni kwa sababu hawezi kumudu kupoteza sura zote hizi na kuwa katika hali ya aibu mbele ya wote ambao wanamuunga mkono."

Finnegan, ambaye alikuwa amesimamishwa upadri kufuatia madai hayo na sasa hatoweza kuruhusiwa kurejea kwenye shirika hilo, alitiwa hatiani na baraza katika mahakama ya Bradford mwezi uliopita.

Wakati wa kesi, alisisitiza hawezi kuwa mdudu wa ngono kutokana na kuwa na ndoa yenye furaha baada ya kuvunja kwa siri kiapo chake kwa kumuoa Beverley Dawson mwaka 1999.

Wawili hao walifunga ndoa nchini Cyprus baada ya kuwa wamekutana katika parokia yake ya zamani huko Castleford, West Yorkshire, ambako bado anaendelea kuishi.

Akitoa ushahidi katika kesi hiyo, Beverley alisema kwamba yeye na mumewe hawakuwahi kuishi pamoja kwa kudumu lakini walionana mara kwa mara, kufanya mahusiano ya kimapenzi na kwenda mapumzikoni pamoja.

Finnegan, ambaye alijiunga na kanisa hilo mwaka 1977, 'alivutiwa kimapenzi' na muathirika huyo, ambaye alitambulishwa mahakamani hapo kama B, na kukiri alikuwa na 'hisia za kimapenzi' kwa mwanafunzi huyo wa kidato cha sita, alisema Thomas.

"Jumapili ya Pasaka, hukuweza kujidhibiti mwenyewe na uliibua vivutio vyako vya kimapenzi kwa B kwa kufanya kosa hili la shambulio la ubakaji," aliongeza.

"Ulisema kwamba ulimpenda na kwa nguvu ukalazimisha kumkumbatia. Uliweka mkono nyuma ya kichwa chake na kwa kutumia mkono wako mwingine ukamshika kwa chini.

"Huku ukiwa umemshika ukarudia rudia kumbusu mdomoni ambapo B alielezea kama '

Baadaye Finnegan alijaribu kumnyamazisha kwa hongo ya 'zawadi nzuri ya siku ya kuzaliwa baadaye mwaka huo', mahakama ilielezwa, lakini binti huyo aliieleza familia yake na mtawa huyo akakamatwa.

No comments: