Thursday, May 2, 2013

"SIJAJA BONGO KUFUATA PENZI LA DIAMOND"...AVRIL

Jana ilikuwa ni birthday ya msanii wa Ogopa Djs ya Kenya, Judith Nyambura Mwangi a.k.a Avril ambaye alitua jijini dar es salaam juzi na sababu ya ujio wake ilikuwa ni vitu vikubwa viwili.

Akihojiwa katika kipindi cha XXL kupitia Clouds fm Avril amesema ujio wake hapa bongo kwanza ni ku-celebrate birthday yake na fans wa Tanzania, na pili ni ku-launch single yake mpya aliomshirikisha Ommy Dimpoz ambaye kwa sasa yuko ziarani barani Ulaya, party ilifanyika usiku wa kuamkia jana (April 30) pale Elements club.

Kuhusiana na maneno ambayo yamekuwa yakisemwa juu ya tetesi za kuwepo kwa mahusiano baina yake na Diamond Platnumz ambaye alimshirikisha Avril katika video ya Kesho, Avril amekana kuwepo kwa uhusiano wowote zaidi ya kuwa marafiki wa kawaida na wa kikazi. "Hakuna kitu chochote kati yangu na diamond  na  sijaja  Tanzania  kufuata  penzi  lake... we are just friends na relationship yetu ni proffesional relationship katika muziki", alisema Avril.

Hii ndo birthday party ya kwanza kwa Avril kufanya, birthdays zake zote zilizopita alikua anasheherekea kwa kuchill tu nyumbani na familia yake.

No comments: