Tuesday, June 18, 2013

Serikali imezuia mazishi ya waliouwawa kwa bomu arusha, polisi wanafukuza watu

Ni simanzi na taharuki kubwa zimetanda katika Jiji la Arusha baada ya Serikali kukataza kusanyiko lolote jambo ambalo limesababisha mazishi ya waliouwawa kwa bomu katika kampeni za udiwani za CHADEMA yasiweze kufanyika maanaa Polisi wanatawanya watu kwa mabomu ya machozi na vipigo.

    Ili kupinga uonevu huu, mabalozi 23 wa CCM huko Arusha wamejitoa katika chama hicho (CCM) na walikuwa watangaze rasmi kujiondoa katika hadhara ya kuaga miili ya marehemu. Jambo hili, kwa kuwa lingekuwa pigo kwa CCM, basi chama hicho pamoja na serikali yake kwa kutumia polisi wamepiga marufuku kusanyiko lolote Arusha.

    Aidha, wananchi wa Arumeru wamefunga barabara na kuanza kuandamana kwenda Arusha Mjini kwa Miguu ili kuupinga uonevu na unyanyasaji dhidi ya wananchi unaofanywa na Serikali ya CHAMA CHA MAPINDUZI.

No comments: