Saturday, June 23, 2012

Mwili Wa Marehemu Willy Edward Utawekwa Kwenye Nyumba Yake Ya Milele Leo Saa 9 Alasiri


MWILI wa aliyekuwa Mhariri Mkuu wa gazeti la Jambo Leo, marehemu Willy Edward utawekwa kwenye nyumba yake ya milele leo saa 9 alasiri katika kiwanja cha nyumba yao eneo la Molotonga, Mugumu Mjini, wilayani Serengeti , mkoani Mara.

Kwa mujibu wa ratiba ya mazishi iliyotolewa na Msemaji wa Familia, George Ogunde, inaeleza kuwa ibada ya mazishi itaanza saa 5 nyumbani kwa mzee Edward Ogunde, itaongozwa na Askofu wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Mara, Hilikia Omindo, Askofu wa Anglikana Dayosisi ya Rorya, John Adiema na Mussa Omboi Mchungaji Msaidizi wa Parishi ya Mugumu.

Baada ya ibada kitakachofuatia ni wananchi kuaga mwili wa mpendwa wetu, marehemu, Willy Edward na hatimaye maziko.

Mkuu wa Mkoa wa Mara ambaye kwa hivi sasa yupo bungeni kushiriki wakati wa kutangazwa kwa Bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI), atatuma mwakilishi kwenye mazishi hayo.

Baadhi ya viongozi wengine watakaoshiriki katika mazishi hayo ni Mkuu wa Wilaya ya Magu, Jacquiline Liana, Mwenyekiti wa CCM, Mkoa wa Shinyanga, Hamis Mgeja na wengine wengi.

Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri, Absalom Kibanda aliwasili jana kwenye msiba akitokea Dar es Salaam, akiwa na Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari ya Dar es Salaam, Jane Mihanji, Mhariri wa Gazeti la Matanzania Jumapili, Revocatus Makaranga na Kulwa Karedia ambaye ni Mhariri Mkuu wa gazeti la kila siku la Mtanzania.

Chanzo:  http://richard-mwaikenda.blogspot.com/

1 comment:

Ivan said...
This comment has been removed by a blog administrator.