Saturday, June 23, 2012

Wolper awindwa alishwe sumu


Imefahamika kuwa kuna kundi la watu linamuwinda kwa udi na uvumba mwigizaji Jacqueline Masawe ‘Wolper’ kwa dhumuni la kumlisha sumu ambayo itakuwa ikimtafuna taratibu hadi imfute juu ya uso wa dunia, Risasi Jumamosi limeinyaka.Akizungumza na mwandishi wetu, rafiki wa karibu wa Wolper aliyeomba hifadhi ya jina lake, alisema kuwa kumekuwa na mazungumzo yanayomhusu staa huyo yanayosikika katika kona mbalimbali kunapokuwa na mastaa wa filamu za Kibongo ambayo yamejaa chuki ndani yake huku kisa kikiwa hakijulikani.

“Ukiniuliza kisa ni nini au kosa la Wolper mpaka sasa siwezi kukwambia kwa sababu sijui ni kitu gani lakini kila kukicha ukikaa mahali na wasanii zitapigwa stori mwisho wataanza kumzungumzia vibaya Wolper.

“Kwa mfano tulipokwenda Moshi na Arusha (wikiendi iliyopita), tukiwa kwenye ndege kuna watu walikuwa wakimsema vibaya sana, tena si kwa sauti ya chini kila mtu alikuwa akisikia, nadhani kuna kitu anatakiwa kukifanya kwa sasa ili ajilinde kwa usalama wake,” alisema rafiki huyo ambaye naye ni muigizaji.

Wolper laivu
Kama ilivyo ada, baada ya kupata maelezo ya chanzo hicho cha habari, Risasi Jumamosi lilimvutia waya Wolper na kumweleza kila kitu ambapo mbali na kukiri kuifahamu ishu hiyo, alikuwa na haya ya kusema:

“Ukweli ni kwamba hali halisi nishaipata kwani kwenye ile ndege waliyopanda, mmoja wa wahudumu ni dada yangu tena wa damu kabisa alikuwa anasikia mazungumzo yote yaliyokuwa yakinihusu.”

Wolper alisema kuwa Waswahili wanasema kuwa jihadhari kabla ya hatari hivyo katika hatua aliyochukua kwa kujihadhari, mojawapo ni hiyo ya kutoacha kinywaji au chakula mezani kisha akakirudia.

“Siwezi kumuamini mtu yeyote katika usalama wangu kwa sasa kwani huwezi kujua moyo wa mtu ni msitu mkubwa sana. Sitathubutu kuacha kinywaji au kitu chochote kinachoingia mdomoni hadharani eti kwa kuwa niliokaa nao ni waigizaji wenzangu, nafanya hivyo kutokana na hali halisi. Inavyoonekana watu wanaumia sana mimi kumiliki BMW X6,” alisema Wolper.

No comments: