Saturday, June 23, 2012

MAMA KANUMBA ANUNUA...


ZIMEKATIKA siku 75 tangu kufariki dunia kwa supastaa wa filamu za Bongo, Steven Charles Kanumba, Aprili 7, 2012. Mama mzazi wa marehemu huyo, Flora Mtegoa mambo yamemnyookea ambapo amenunua jumba kubwa la kifahari, Risasi Jumamosi linakuwa la kwanza kuripoti.

CHANZO CHATEMA NYETI
Kwa mujibu wa chanzo cha uhakika, mjengo huo upo Kimara Temboni jijini Dar es Salaam ambapo mama huyo na familia yake (akiwemo Seth Bosco) wamehamia.

Sanjari na wao, pia magari matatu ya marehemu, Toyota Hiace, Toyota Lexus na Toyota GX 110 yamepiga kambi huko, kila moja likiwa na sehemu yake ya kuegesha.

Kwa mujibu wa chanzo hicho, kwa sasa mama Kanumba hana makazi tena pale Sinza Kijiweni ambako ndiko palipofanyikia msiba wa mwanaye hadi kuhitimisha na arobaini yake.

KUNA USIRI
Chanzo kikadai kuwa kuhama kwa mama huyo na familia yake kutoka Sinza kwenda Temboni kumegubikwa na usiri bila kufafanua siri hiyo inatokana na nini!

MAPAPARAZI WAINGIA MZIGONI KUCHUNGUZA
Baada ya gazeti hili kuzidaka nyeti hizo, Alhamisi ya Juni 21, 2012 lilituma timu ya waandishi wake kwenda kupata uhakika wa madai hayo na kujiridhisha kabla ya gazeti halijakwenda mitamboni.

NJE YA NYUMBA
Ndani ya geti kuu la nyumba hiyo yenye bati la kijani, alikutwa mdogo wa marehemu Kanumba, Seth Bosco akipata chai huku upepo mwanana ukimpuliza. Mama Kanumba alikuwa akiendelea na shughuli zake za kawaida.

Mbali na kuwaona wawili hao, mapaparazi wetu waliendelea na uchunguzi wao ambapo waliipiga raundi nyumba hiyo na kujionea magari yote matatu ya marehemu  yakiwa yamepaki huku jamaa mmoja akiwa juu ya bati kuweka dishi la televisheni la ‘kuangalizia’ Mashindano ya Kombe la Mataifa ya Ulaya ‘Euro’ yanayoendelea kwa sasa nchini Poland na Ukraine.

Makachero wetu walipojiridhisha kuwa mama Kanumba ndiyo kaweka makazi yake mapya, lilipiga picha za kumwaga kisha lilimwendea hewani Seth na kuzungumza naye ili kupata ukweli mwingine.

SAUTI YA SETH KUTOKEA TEMBONI
Paparazi: Mambo Seth?
Seth: Poa tu, nani mwenzangu?
Paparazi: Unaongea na Risasi Jumamosi hapa.
Seth: Enhe, lete habari.

Paparazi: Inasemekana mmehama pale Vatican, mmehamia wapi?
Seth: Aaa, tumehamia Temboni huku.
Paparazi: Ni kweli huko mmenunua nyumba?
Seth: Ni kweli.

Paparazi: Shilingi ngapi?
Seth: Mh! Hilo swali anayeweza kujibu ni mama kwamba ni shilingi ngapi na mambo mengine yote.
Risasi Jumamosi lilipomsaka mama Kanumba kwa kutumia simu yake ya mkononi, hakupatikana hewani siku hiyo.

MJENGO WA BEI MBAYA
Hata hivyo, Risasi Jumamosi lilifanya uchunguzi na kunyaka baadhi ya nyaraka zinazoonesha kuwa mjengo huo umenunuliwa kwa shilingi milioni themanini (80,000,000) za Kibongo.

MASTAA HAWAJUI
Gazeti hili lilijaribu kufanya mawasiliano na baadhi ya mastaa wa filamu Bongo kama wanajua mama yao huyo amehama Sinza lakini kila aliyeulizwa hakuwa anafahamu na kuwa ‘sapraizi’ kwake.
Mwanyekiti wa Klabu ya Bongo Movie, Jacob Steve ‘JB’ alipovutiwa uzi na kuulizwa alisema hajui kama mama Kanumba amehama Sinza.
HII HAPA SAUTI YAKE
“Amehama pale? Duu! Mimi sijui kaka.”

MWAKIFAMBA AKIWA NJIANI KWENDA SINZA
Naye Mwenyekiti wa Shirikisho la Filamu Bongo, Simon Mwakifamba alipopigiwa simu kuulizwa, akajibu anaamini mama huyo bado yupo Sinza, na yeye mwenyewe alipanga kwenda siku hiyo ya Alhamisi jioni ili akamjulie hali. pisha zaidi - globalpulishershttp://www.globalpublishers.

No comments: