Sunday, August 19, 2012

'Baby J' ahamishia MABEGI Dar!


Toka kisiwani Zenji,  mwanadada anayefanya vyema kwasasa kwenye ramani ya muziki wa kizazi kipya Baby J, ameamua kuhamishia makazi yake  jijini Dar,  huku akielezea sababu ya kufanya hivyo ni kutafuta soko zuri la muzuki wake.

Kauli ya msanii huyo inaweza kuwa sawa na mwezake AT, ambaye amehamia rasmi dar kwa kufuata soko analoamini kuwa ni bora.

Hata hivyo Baby J alisema haoni sababu ya kutowashukuru mashabiki wake wa Visiwani na Bara kwa kumpa sapoti katika kila wimbo ambao amekuwa akitoa.

“Dar nimekuja kufanya muziki na kuchukua nafasi hivyo naamini sapoti kubwa ninayopata kutoka mashabiki ndiyo inayonipa nguvu ya kuendelea kufanya kazi hivyo nawaahidi wale wote wanaopenda kazi zangu ni kwamba sitawaangusha kabisa,” aliongeza.

No comments: