Sunday, August 19, 2012

Mpinzani wa Wolper huyoo


Jasmin alisema kwamba toka anaanze kuigiza filamu zote, watayarishaji wamekuwa wakimkubali nakusema kwamba yeye uwezo wake ni mkubwa na anaweza kabisa kumpoteza Jacqueline Wolper.

Alisema Wolper ni mmoja kati ya wasanii wanaomvutia sana, yeye  na wasanii wengine kama Monalisa na Msanii Johari kwani hiyo yote ni kutokana na kupitia kazi zao.

Mbali na hilo alisema kwamba haofii ushindani, bali siku ya siku anatarajia kukimbiza wasanii wenzake kwenye sanaa ya Filamu hapa nchini.

Si mwingine bali ni yule Mwigizaji wa kike anayekuja wka kasi ya ajabu kwenye sanaa ya Filamu Swahiliwood Neema Oberlin Kimaro ‘Jasmin’, huenda akawa tishio kwa msanii anayeng'ara kwa sasa kwenye sanaa ya Filamu ambaye ni Jaqueline Wolper Massawe.

Mbali ya kuwa ni msanii anayetoka Mkoani Kilimanjaro anakotoka mpinzani wake Jack, kwa muda mfupi sasa toka aingie kwenye sanaa hiyo ya Filamu  ameonyesha uwezo mkubwa baada ya kushiriki kwenye Filamu ya Essau Hellen akiwa mhusika mkuu katika filamu hiyo.

Mara  nyingi  vipaji vya wasanii vimekuwa vikiibuliwa, lakini msanii huyu ameonyesha uwezo wa hali ya juu sana kwenye Filamu ya Essau Hellen na amecheza kama mhusika mkuu akiigiza kwa kutumia jina la Jasmin nafasi ambayo imechezwa na wahusika wawili yeye na msanii mkongwe Grace Mapunda (Mama Kawele).

No comments: