Sunday, August 19, 2012

Ofisi ya madame Rita yateketea kwa moto


Ijumaa ya August 17 2012 na ijumaa nyingine kabla ya hii ya August 17 zimekua siku mbaya kwa Madame Rita Paulsen Big boss wa Benchmark Production ambayo ndio muandaji wa mashindano ya Bongo star search.

August 17 shoti ya umeme imemsababishia hasara sio chini ya milioni hamsini za kitanzania baada ya nyumba iliyokua inatumika kama stoo ya vifaa vya production Benchmark kuteketea yote kwa moto pamoja na vitu vilivyokuwemo ndani.

Madame amesema shoti ya umeme ilitokana na transfoma ambayo ipo karibu na ofisi yao Kawe Dar es salaam ambapo ofisi yote ilikua iungue ila shoti ilipofika kwenye ofisi kubwa umeme ulijizima wenyewe kutokana na vifaa kifaa maalum kinachoweza kuzuia shoti, hivyo nyumba ndogo ya stoo iliyokua na vifaa vya productions vilivyokua vinatumika kwa miaka kumi Benchmark production ndio ikateketea.

Tanesco wamethibitisha kweli kwamba ajali ya moto imetokana na shoti ya umeme ambapo zimamoto walichelewa kufika kwenye eneo la tukio kwa zaidi ya saa moja na nusu huku wakisema foleni barabarani ndio iliyosababisha, hakukua na njia ya kuuzima huo moto hivyo Madame Rita na timu yake walibaki wakitazama tu nyumba ikiteketea.

Nilipomuuliza Madame kuhusu msg niliyotumiwa ya uwezekano wa BSS kusimamishwa kutokana na hiyo ajali ya moto, namkariri akisema “nahisi huyo jamaa labda alikua anataka hivyo lakini BSS haiwezi kusimama kuruka hata siku moja, hata nikifariki”


Madame Rita. Amesema anategemea wenye nyumba hiyo watakua wana insurance.

Kuhusu tukio la ijumaa iliyopita kabla ya hii ya August 17, Madame Rita amesema “wezi waliniibia begi langu lenye vitu vingi vya thamani, shilingi milioni tatu pamoja na kadi za benki, vitambulisho na funguo za gari Mercedes Benz ambayo mpaka sasa haliwezi kuwaka kwa sababu ufunguo ndio nilikua nao huo huo wa spea hivyo ilibidi libebwe mpaka nyumbani, walinipokonya wakati nimesimama nazungumza na mtu”

Madame alisha ripoti polisi lakini mpaka sasa hajapata chochote kati ya vilivyoibiwa, ameomba yeyote anaehusika arudishe tu hizo funguo hata kwenye ofisi za Clouds Fm mikocheni, aweke kwenye bahasha na hata akiandika Millard Ayo zitamfikia kwa sababu anashindwa kulitumia gari sasa hivi na inambidi aagize funguo mwingine kwenye kampuni ya Benz Ujerumani kitu ambacho kitatumia muda mrefu.
Chanzo:Millard Ayo.com

No comments: