Saturday, September 1, 2012

SACCO - Yapatiwa Mkopo Wa Matrekta Na Benki Ya Raslimali-TIB

 Matrekta 11  yaliyotolewa mkopo kwa wanachama wa Talanta SACCOS ya tarafa ya Kinyangiri wilaya ya Mkalama Mkoani Singida.
 Mkuu wa mkoa wa Singida,Dk.Parseko Kone, akizungumza na wananchi kisha alikabidhi matrekta makubwa 11 kwa wanachama wa Talanta SACCOS ya tarafa ya Kinyangiri wilaya Mkalama, yaliyotolewa mkopo na Benki ya rasilimali (TIB), kwa gharama ya Sh.Milioni 450.5.
 Mwenyekiti wa Talanta SACCOS tarafa ya Kinyangiri Mayasa Salum,akifurahia trekta alilokopeshwa na benki ya rasilimali (TIB), kupitia SACCOS hiyo
MKUU wa mkoa wa Singida Dk.Parseko Kone akikaribishwa na mmoja wa wanachama wa ‘Talanta SACCOS’ katika kijiji cha Iguguno tarafa ya Kinyangiri wilaya ya Mkalama alipoenda kukabidhi matrekta 11 yaliyogharimu Sh. Milioni 450.5.

Wananchi wametakiwa kujiunga katika vikundi ili kunufaika na mikopo inayotolewa nataasisi za vyombo vya kifedha. Mkuu wa mkoa wa Singida,Dk.Kone,alisema hayo wakati wa kukabidhi matrekta makubwa 11 kwa Talanta SACCOS ya tarafa ya Kinyangiri, wilayani Mkalama, yenye thamani ya Sh. Milioni 450.5 kutoka benki ya raslimali (TIB). Dk. Kone alisema kupitia ushirika wakulima na wananchi kwa ujumla watanufaika na mkakati wa kilimo kwanza.Kwa upande wake mwenyekiti wa Talanta SACCOS, Myasa Salum aliishukru benki hiyo ambayo imelenga kumkomboa mkulima wa kawaida kijijini.

Na: Elisante John,Singida

No comments: