Saturday, September 1, 2012

TANAPA Waunda Kikosi Kazi Kupambana Na Ujangili Wa Watalii Na Wanyama

Shirika la hifadhi za taifa(Tanapa) na mamlaka ya hifadhi za Ngorongoro (Ncca) wakishirikiana na Jeshi la Polisi wameunda kikosi kazi katika vita ya kupambana na ujangili na uhalifu kwenye mbuga za Ngorongoro.Manyara,Tarangire na Serengeti katika kudhibiti ongezeko la ujangili haramu kwenye mbuga hizo.

Akizungumza na waandishi wa habari Ofisini kwake Kamanda wa upelelezi mkoa wa Arusha Kamilus Wambura alisema kwamba kama hatutatumia kikamilifu wimbi la vurugu zinazotokea kwa wenzetu wan chi ya jirani na watalii wengi kuhamia nchini kwetu kwa kuweka ulinzi shirikishi kati yetu na mamlaka za hifadhi ya wanyama pori basi badala ya watalii hao kuja watatukimbia hivyo kupoteza mapato kwa taifa letu.

Wambura alisema kuwa watanzania wamejaaliwa kuwa na mbuga nzuri zenye vivutio na wageni wengi sasa wanakuja kutembelea mbuga hizo ukifika kwenye hotel zetu huko mbugani kwa siku hadi wageni 900 wanalala kama hatukuwalinda mali zao na usalama wao watatukimbia.

“Wageni hawa ni wengi sana ndugu waandishi tunatakiwa kuwalinda wao na mali zao ilikuwa mabalozi wazuri wa kuitangaza Tanzania huko kwao na kueleza mazuri ya nchi yetu kuwa ni mahala salama kwao na malizao”alisema Wambura.

Hivyo tumeunda kikosi kazi katika kulinda wanyama wetu na wageni wetu wanaotembelea mbuga zetu ili kuweza kupata wageni zaidi watakao kuja kutembelea mbuga zetu na kuongeza mapato ya taifa kwa ujumla na kuona Tanzania ni mahali salama pa kutambelea.

Tunaomba pia ushirikiano wenu na wananchi wa maeneo yanayozunguka mbuga hizo na nyingine kutoa taarifa za ujangili au kuwepo tetesi zozote za kuwepo majangili na majambazi ilikurahisisha zoezi hili wanyama ni tunu tuliojaaliwa na mungu tunaowajibu wakuilinda.

Hebu fikiri mnyama kama Tembo ukubwa wake halafu anauawawa kwa ajili ya vipembe vidogo tu tuwe na huruma kwa wanyama na mbuga zetu sisi polisi na mamlaka husika tutawalinda kwa nguvu zetu zote.

No comments: