Saturday, September 1, 2012

Zoezi La Sensa Kumalizika Tarehe 8 Septemba 2012

 Kamishna wa Sensa wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS)  Hajjat Amina Mrisho Said akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam kuhusu zoezi la Sensa ya watu na makazi 2012  linaloendelea nchi nzima na kutoa wito kwa wananchi ambao bado hawajahesabiwa kutoa taarifa kwa viongozi wa serikali za mitaa.
Waandishi wa habari wakimsikiliza Kamishna wa Sensa wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Hajjat Amina Mrisho Said (hayupo pichani) leo jijini Dar es salaam wakati akitoa taarifa ya kuongezwa kwa muda wa zoezi la Sensa ya watu na makazi litakalomalizika tarehe 8 Septemba 2012.

 Picha na Aron Msigwa - MAELEZO.

No comments: