Friday, January 4, 2013

TANAPA WAONGEZA MUDA WA KUWASILISHA KAZI ZA KUSHINDANIWA



Kutokana na changamoto mbalimbali zilizojitokeza na kuibuliwa na wadau wa habari nchini kuhusiana na siku ya mwisho ya kuwasilisha kazi za kushindaniwa, Waandaaji wa TANAPA Media Awards 2012 wamesogeza mbele tarehe ya mwisho ya kuwasilisha kazi hizo kutoka 31.12.2012 na kuwa tarehe ya mwisho sasa itakuwa 31.01.2013.

WASHIRIKI:

Tuzo hizi ziko wazi kwa wanahabari wote nchini kutoka katika Magazeti, Redio na Runinga. Ili uweze kutimiza sifa za ushiriki wako katika tuzo za TANAPA Media Awards 2012, unatakiwa kuwasilisha kazi zote zilizochapwa na kutangazwa katika kipindi cha kuanzia tarehe 01 Januari, 2012 hadi 31 Disemba, 2012.

JINSI YA KUSHIRIKI

Wanahabari wanaweza kushiriki kwa kutuma kazi zao kwa kiwango cha juu cha kazi tatu kwa kila kundi. Wanahabari watakaoshiriki tuzo hizi watapaswa kujaza fomu maalum za ushiriki zinazopatikana katika tovuti ya shirika www.tanzaniaparks.com

MAKUNDI

A     Tuzo ya Utalii wa Ndani katika Hifadhi za Taifa     Redio                 (washindani watatu)
Runinga             (washindani watatu)
Magazeti            (washindani watatu)
B     Tuzo ya Uhifadhi katika Hifadhi za Taifa     Redio                 (washindani watatu)
Runinga             (washindani watatu)
Magazeti            (washindani watatu)

Kazi zinaweza kuwasilishwa katika lugha ya kiingereza au Kiswahili. Tuzo: Washindi kwa kila kundi watapata tuzo zifuatazo:

Mshindi wa Kwanza    

Fedha taslimu Sh. 1,500,000, Ngao, Cheti na Safari ya mafunzo katika moja ya nchi za SADC
Mshindi wa Pili    

Fedha taslimu Sh.1,000,000, Ngao na Cheti
Mshindi wa Tatu    

Fedha taslimu Sh.500,000 na Cheti

Mwisho wa kuwasilisha

Kazi zote zinatakiwa kuwa zimewasilishwa Makao Makuu ya TANAPA hadi kufikia tarehe 31.01.2013.

Anuani ya kuwasilisha kazi:

Mkurugenzi Mkuu

Hifadhi za Taifa Tanzania

AIONE: Meneja Uhusiano- TANAPA Media Awards 2012

SL.P. 3134

Arusha, Tanzania

Au, ziletwe kwa mkono Makao Makuu ya TANAPA, Barabara ya Dodoma, Chumba Namba.32.

Au barua pepe:        prm@tanzaniaparks.comImetolewa na

Pascal Shelutete

MENEJA UHUSIANO

HIFADHI ZA TAIFA TANZANIA

04.01.2013

No comments: