Friday, January 4, 2013

TEKELEZENI AHADI MLIZOZITOA WAKATI WA KUOMBA KURA-OLE NANGOLE

 MWENYEKITI wa Chama cha Mapinduzi mkoa wa Arusha(CCM)Bw Onesmo Ole Nangole amewataka Viongozi mbalimbali wa chama hasa wale ambao walitoa ahadi  kwa wananchi kwenye uombaji wa kura kuhakikisha kuwa wanatekeleza ahadi hizo kwa haraka sana kwani wale ambao hawatekelezi ahadi wanachangia sana chama hicho kuelekezewa lawama

 Bw. Nangole aliyasema hayo Juzi wakati akifungua Kata mpya ya Chama hicho ambayo kwa sasa inajulikana kama Kata ya Majengo iliopo Meru Mkoani Arusha.

 Aidha Bw Nangole alisema kuwa tabia ya baadhi ya Viongozi ya kuwa watoa ahadi hasa nyakati za kura na kisha wakishapata kura wanasahau ahadi zao inachangia sana kuunguza Ccm kwenye jamii na kuonekana kuwa ni watoaji ahadi zisizotekelezwa.

 Alisema kuwa Viongozi wote ambao walitoa ahadi mbalimbali kwa wananchi hasa katika Nyakati za Kura wanatakiwa kuhakikisha kuwa watekeleza ahadi zao na kujijengea tabia ya kuwaangalia wapiga kura wao ili kuendelea kulinda uhai wa Chama

 Mbali na hayo aliongeza kuwa Viongozi mbalimbali wa Chama hicho wanatakiwa kuangalia zaidi ilani ya chama hicho kwa kuhakikisha kuwa wanaainisha matatizo ambayo yapo kwenye jamii na kisha kuyatatua kuanzia kwenye Ngazi za Vitongoji na Vijiji.

 Katika hatua nyingine Katibu wa Chama hicho Wilaya ya Meru Bw Langaeli Akyoo alisema kuwa bado Wilaya hiyo inakabiliwa na changamoto mbalimbali ambazo zinatakiwa zitatuliwe kwa haraka sana ingawaje umoja na ushirikiano unaitajika kwa haraka sana

No comments: