Friday, January 4, 2013

SAJUKI AMWACHIA DINO WOSIA MZITO

BAADA ya kutokea kwa kifo cha staa wa filamu za Kibongo, Juma Kilowoko ‘Sajuki’ (27), rafiki yake mkubwa ambaye mwigizaji mwenzake, Denis Sweya ‘Dino’ (pichani juu) amefunguka kuwa ameachiwa wosia mzito juu ya mke wa msanii huyo, Wastara Juma na mwanaye.

Akizungumza kwa uchungu msibani nyumbani kwa mastaa hao Tabata, Dar, Dino alisema yeye na Sajuki urafiki wao ulikuwa ni kama ndugu hivyo walikuwa karibu kila sehemu ambapo siku za hivi karibuni msanii huyo alimweleza juu ya mkewe Wastara na mwanaye kwamba alishamwambia mama yake mzazi kuwa hata akiwa hayupo duniani, wasimsumbue, wamwache amlee mtoto wao katika malezi bora kwani anampenda kupita maelezo.

“Mimi na Sajuki tulikuwa marafiki sana na tulipanga mambo mengi kuhusu kazi. Kila alipokuwa anakaa alikuwa aniambia kuwa anamuomba Mungu apone haraka tufanye kazi ya nguvu itakayoshangaza ulimwengu lakini malengo yetu hayakutimia, Mungu amemchukua,” alisema Dino.

Kwa upande mwingine alisema kuwa anawashangaa wasanii wanaokaa na kupiga majungu kwani wanachofanya ni ujinga ambao hauna maana kwani tayari Sajuki amefariki na huu ni mwaka mpya lakini wao bado wanaendekeza vinyongo walivyokuwa navyo mwaka jana.

Stori:  Gladness Mallya

No comments: