Saturday, April 13, 2013

KITENDO CHA KUWANYANG'ANYA ARDHI WANANCHI WA LOLIONDO CHAMCHANGANYA RAIS KIKWETE

Sakata la mgogoro unaorindima kwa sasa kuhusu unyang'anywaji wa Ardhi ya Loliondo kwa lengo la kumpa mwekezaji wa kiarabu umemvuruga sana Rais Kikwete na kusita kujitokeza hadharani kulitolea kauli.

Hapo awali Kupitia kikao cha baraza la mawaziri iliamriwa kuwa WAKAZI WA LOLIONDO WANYANG'ANYWE ENEO HILO na kumtuma Waziri wa Maliasili na Utalii Hamisi Kagasheki kwenda kulisimamia kwa nguvu zote....

Lakini Kauli ya hivi karibuni iliyotolewa rasmi na CCM kupitia kwa Naibu katibu mkuu wake Mwigulu Nchemba ambaye alitumwa na Secretariety ya CCM akiwa kama mjumbe mkuu wa kamati maalum aliyotumwa kwenda Loliondo kujaribu kutafuta suluhu kwa njia za Kisiasa ya kuwa 'WANANCHI WA LOLIONDO WANA HAKI NA ARDHI YAO NA WAZIRI KAGASHEKI ALIKOSEA KATIKA MAAMUZI YAKE YA KUTAKA KUWANYANG'ANYA ENEO HILO' imemchanganya zaidi rais Kikwete kwa kuwa yeye pia ni mwenyekiti wa CCM na hata mtu aliyewahi kutoa Kibali cha kisheria cha umiliki wa Ardhi hiyo wa wakazi wa Loliondo alikuwa pia waziri wake!!

Habari za ndani kabisa zinasema kuwa, Rais alikuwa tayari ameamua kumtuma Waziri mkuu Pinda kwenda Loliondo ama kupitia Bunge Kutoa Kauli juu Mgogoro wa Loliondo lakini dakika za mwisho mwisho Pinda alizuiwa(Alikataa?) kufanya jambo lolote maana ingechafua Upepo wote, badala yake Alitumwa Kagasheki aendelee kufa nalo huku Serikali ikipima upepo!!

No comments: